Vietnam yakaribisha makundi ya kwanza ya watalii wa China katika kipindi cha miaka mitatu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 17, 2023
Vietnam yakaribisha makundi ya kwanza ya watalii wa China katika kipindi cha miaka mitatu
Wafanyakazi wa Vietnam, wakiwa wameshika mashada ya maua ili kuwakaribisha watalii wa China kwenye Lango la Mpaka wa Kimataifa wa Huu Nghi katika jimbo la Lang Son, Kaskazini mwa Vietnam, Machi 15, 2023. (Xinhua/Hu Jiali)

HANOI - Mamlaka ya utalii ya Vietnam na kamati ya umma ya Jimbo la Lang Son, Kaskazini mwa nchi hiyo zimefanya hafla siku ya Jumatano kukaribisha makundi ya kwanza ya watalii wa China katika miaka mitatu iliyopita tangu janga la UVIKO-19.

Makundi hayo ya watalii yenye jumla ya watu 120 wa China yalipokelewa kwenye Lango la Mpaka wa Kimataifa wa Huu Nghi kwa zawadi nzuri na maonesho ya michezo ya Sanaa ya kijadi.

Deng Guilin, mtalii mwenye umri wa miaka 67 ambaye anatoka katika Jimbo la Hubei la China, amesema hii ni mara yake ya kwanza kufika Vietnam. Amepanga kutembealea Hanoi, mji mkuu wa Vietnam, na Ghuba ya Halong katika Jimbo la Quang Ninh "kujionea uzuri wa mji wenye umri wa miaka 1,000 na Eneo la Urithi wa Dunia la UNESCO huko Vietnam."

Peng Shituan, konseli wa utamaduni wa Ubalozi wa China nchini Vietnam, amesema kuwa hafla hiyo ni wakati wa kihistoria wa kuanza tena ushirikiano wa kitalii kati ya China na Vietnam.

Peng amesema, "Kila mtalii wa China ni balozi wa kati ya watu wa urafiki wa China na Vietnam," na shughuli za utalii zimefanya kazi muhimu katika kukuza mabadilishano kati ya watu wa nchi hizo mbili majirani.

"Ushirikiano wa utalii ni sehemu muhimu ya ushirikiano kati ya Vietnam na China. Sekta ya utalii ina maana kubwa kwa Vietnam kwani kurudi kwa watalii wa China kutachangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa Vietnam 2023," Ha Van Sieu, Naibu Mkuu wa Idara ya Kitaifa ya Utalii yaVietnam ameliambia Shirika la Habari la Xinhua.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha