Maua ya Bingling yavunja barafu na kuchanua Heilongjiang, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 17, 2023
Maua ya Bingling yavunja barafu na kuchanua Heilongjiang, China

Hivi karibuni, maua ya Bingling yamechanua moja baada ya lingine kwenye barafu katika Bustani ya Kitaifa ya Misitu ya Mudanfeng katika Mji wa Mudanjiang wa Mkoa wa Heilongjiang wa China, yakivutia watalii wengi kwenda huko kuyaangalia na kupiga picha.

Inafahamika kwamba, maua ya Bingling, ambayo pia huitwa maua ya karibisha majira ya mchipuko, ni maua ya kwanza kuchanua Kaskazini mwa China wakati wa majira hayo yenye baridi. Maua ya Bingling ya Bustani ya Mudanfeng kwa kawaida huchanua Mwezi Machi wa kila mwaka, na hufikia kilele chake cha kuchanua katikati mwa Mwezi Aprili. Maua hayo yenye rangi ya dhahabu huvunja barafu ili kuchanua, na huleta mandhari nzuri ya kuvutia kwenye mazingira yenye theluji nyeupe.

Picha zimepigwa na Qu Bo, Wang Geng, Wang Jilei. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha