Wakulima waotesha miche “hewani” katika Mkoa wa Henan, China (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 17, 2023
Wakulima waotesha miche “hewani” katika Mkoa wa Henan, China
Mkulima akiangalia na kutunza miche ya mpunga unaoweza kupata mavuno mara mbili kwenye kiwanda cha kiotomatiki cha kuotesha miche kwa kutumia teknolojia za akili bandia cha Ushirika wa Qinglonghe wa Kijiji cha Zhanglou katika Mji wa Xinyang, Mkoa wa Henan nchini China. (Picha zilipigwa na Xie Wanbai)

Tarehe 15, Machi, wakulima waliangalia na kutunza miche ya mpunga unaoweza kupata mavuno mara mbili kwenye kiwanda cha kiotomatiki cha kuotesha miche kwa kutumia teknolojia za akili bandia cha Ushirika wa Qinglonghe wa Kijiji cha Zhanglou katika Mji wa Xinyang, Mkoa wa Henan nchini China. Hivi sasa ni wakati wa kilimo cha majira ya mchipuko na kujiandaa kupandikiza miche. Wakulima wa kijiji hicho wamehamisha mashamba ya kuotesha miche kutoka “ardhi” mpaka “hewani”, na kutoka nje mpaka ndani. Wanatumia teknolojia kuotesha miche kwenye kiwanda cha kiotomatiki cha kuotesha miche kwa kutumia akili bandia, hali ambayo imeongeza ufanisi na ubora wa uoteshaji wa miche.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha