Mchoro kamili wa zodiac wagunduliwa katika hekalu la Enzi ya Warumi, Kusini mwa Misri

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 20, 2023
Mchoro kamili wa zodiac wagunduliwa katika hekalu la Enzi ya Warumi, Kusini mwa Misri
Picha hii isiyo na tarehe ikionyesha ukuta wenye michoro, ambayo ni sehemu ya michoro ya zodiac iliyogunduliwa kwenye dari ya Hekalu la Esna huko Luxor, Misri. (Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale ya Misri/Xinhua)

CAIRO  Mchoro kamili wa zodiac    umegunduliwa kwenye dari ya hekalu la Enzi ya Warumi katika Jimbo Luxor, Kusini mwa Misri, Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale ya nchi hiyo imesema Jumapili.

Ukuta wa zodiac, pamoja na michoro na michongo ya wanyama na miungu ya kale, iligunduliwa na timu ya warejeshaji wa vitu vya kale ya Misri wakati wa kazi ya pamoja ya Misri na Ujerumani ya kurejesha vitu vya kale kwenye Hekalu la Esna.

“Ugunduzi huo unaifanya Esna kuwa hekalu la pili la kale nchini humo kuwa na mchora kamili wa zodiac, baada ya picha nyingine mbili zilizopatikana katika hekalu la Dendera huko Qena,” wizara hiyo imesema katika taarifa.

Wizara hiyo imeongeza kuwa, kuanzishwa na michoro ya Hekalu la Esna kulikamilika katika Mwaka 250 A.D wakati Misri ilipotawaliwa na Dola ya Kirumi.

Hekalu hilo lenye ukumbi mmoja lina nguzo 24 zenye maandishi na michoro inayoonyesha wafalme wa wakati wa Ptolemaic wa Misri na wafalme wa Roma.

 

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha