Yakichukua "kasi ya biashara ya mtandaoni" Mawigi ya China yauzwa vizuri nje ya nchi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 20, 2023
Yakichukua
Wafanyakazi wakitengeneza mawigi kwenye karakana ya uzalishaji ya Kampuni ya Bidhaa za Nywele ya Rebecca katika Mkoa wa Henan, China, Tarehe 16, Machi.

Katika miaka ya hivi karibuni, kampuni zinazojihusisha na biashara ya bidhaa za nywele katika Mji wa Xuchang, Mkoa wa Henan, China zimefanya juhudi za kutafuta njia za kuuza bidhaa kwa matangazo ya moja kwa moja mtandaoni katika biashara ya mtandaoni ya kuvuka mipaka na ya ndani ya nchi, kuanzisha timu za kitaaluma zinazoshughulika na kuuza bidhaa kupitia jukwaa la biashara ya mtandaoni, na kupanua njia za mauzo. Bidhaa zake zimeuzwa kwa zaidi ya nchi na maeneo 150 kupitia jukwaa la biashara ya mtandaoni. Kufuatia kuongezeka kwa idadi ya oda za mtandaoni, bidhaa za aina zote za nywele zinazopendwa zikitumia fursa ya "kasi ya biashara ya mtandaoni" zinapeleka rangi nzuri duniani. (Picha na Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha