Panda wapendwa waliopo Russia wavutia watalii wengi mfululizo (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 20, 2023
Panda wapendwa waliopo Russia wavutia watalii wengi mfululizo
(Picha ilipigwa na Weng Qiyu/People's Daily Online)

Tarehe 19, Machi, 2023 kwa saa za Moscow, watalii wengi walifika Bustani ya Wanyama ya Moscow kwa ajili ya kutazama panda “Ruyi” na “Ding Ding”. Inafahamika kwamba, jumba hilo la panda limekuwa eneo linalopendwa zaidi na wakazi na watalii katika Bustani ya Wanyama ya Moscow kwa miaka minne mfululizo.

Panda dume “Ruyi” alizaliwa kwenye msingi wa Bonde la Bifengxia wa Ya’an wa Taasisi ya Uhifadhi na Utafiti wa Panda ya China mwezi wa Julai, 2016, na panda jike “Ding Ding” alizaliwa kwenye msingi wa Shenshuping Wolong wa Taasisi hiyo mwezi wa Julai, 2017. Mnamo Mwaka 2019, wakati ambapo uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Russia ulitimiza miaka 70, mapacha hao “wajumbe wa urafiki” walikwenda Russia, na wataishi katika nchi hiyo kwa miaka 15. (Weng Qiyu/People’s Daily Online)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha