Mbio za Marathon za Kampuni ya Magari ya Changan za Chongqing Mwaka 2023 zafanyika kwa shauku kubwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 20, 2023
Mbio za Marathon za Kampuni ya Magari ya Changan za Chongqing Mwaka 2023 zafanyika kwa shauku kubwa
(Picha na CMSports)

Saa moja asubuhi, Tarehe 19, Machi, Mbio za Marathon za Kampuni ya Magari ya Changan za Chongqing Mwaka 2023 zilianza katika Barabara za Nanbin na Babin huko Chongqing, China. Washiriki 30,000 kutoka miji 347 duniani kote walishiriki kwenye mashindano hayo. Naibu Meya wa Serikali ya Manispaa ya Chongqing,Dan Yanzheng, katibu wa Kamati ya Chama na makamu mwenyekiti wa Shirika la Riadha la China, Wang Nan, na viongozi wengine na wawakilishi wa wadau walihudhuria hafla za ufunguzi na kufyatua bunduki kuashilia kuanza kwa tukio hilo.

Baada ya mchuano mkali, ANDERSON SAITOTI SEROI kutoka Kenya alishinda ubingwa wa marathon kwa wanaume kwa kukimbia kwa muda wa saa 2, dakika 11 na sekunde 55. GIZACHEW HAILU NEGASA kutoka Ethiopia alishinda nafasi ya pili kwa kukimbia kwa muda wa saa 2, dakika 11 na sekunde 57. Nafasi ya tatu ilichukuliwa na MENGISTIE ASREN GETAW kutoka Ethiopia ambaye alikimbia kwa muda wa saa 2, dakika 12 na sekunde 13.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha