Picha: Daraja la upinde kubwa zaidi duniani linalojengwa mkoani Guangxi, China (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 21, 2023
Picha: Daraja la upinde kubwa zaidi duniani linalojengwa mkoani Guangxi, China
Picha hii ikionyesha eneo la ujenzi wa Daraja Kubwa la Tian’e Longtan. (Picha na Chen Guanyan)

Daraja Kubwa la Tian'e Longtan ni mradi wa udhibiti wa barabara ya mwendo kasi kutoka Nandan hadi Tian'e Xialao. Daraja hilo lina urefu wa mita 2,488.55. Daraja kuu ni la muundo wa upinde linalojengwa kwa zege nzito, na umbali kati ya mihimili yake miwili ni wa mita 600. Litakapokamilika, litakuwa daraja kubwa zaidi kuliko Daraja la Pingnansanqiao (lenye urefu wa mita 575) na kuwa "Daraja la Upinde la kwanza duniani". Ujenzi wa daraja hilo unatarajiwa kukamilika na kuzinduliwa mwishoni mwa mwaka huu. (Picha na Chen Guanyan)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha