Njia ya kale ya China ya kupanda mbegu kwa kutumia punda yaleta mafanikio

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 22, 2023
Njia ya kale ya China ya kupanda mbegu kwa kutumia punda yaleta mafanikio
Picha iliyopigwa angani ikionesha mashamba ya matuta ya mawe kwenye eneo kame katika Wilaya ya Shexian ya Mkoa wa Hebei wa China. (Picha inatoka ChinaDaily)

Kama walivyofanya wanakijiji wengine wengi wa Wilaya ya Shexian, mkulima Cao Tinghuai kila mwaka anasherehekea siku ya kuzaliwa ya punda wake, ili kumshukuru punda huyo kwa msaada wake shambani.

“Punda ni sehemu muhimu ya maisha yetu, ni kama mwana familia wetu. Kwa hivyo nimempikia tambi za kutengenezwa nyumbani ili kumshukuru kwa kutusaidia kwa bidii kubeba mizigo na kulima mashamba” anasema Cao mwenye umri wa miaka 67.

Katika Wilaya ya Shexian ya Mkoa wa Hebei, Kaskazini mwa China, punda hufanya kazi muhimu katika mfumo wa kilimo milimani wenye historia ya miaka 700. Mfumo huo umetambuliwa duniani kwa ufanisi endelevu wa kuunganisha mambo ya jadi na uvumbuzi.

Mashamba ya matuta ya Wilaya ya Shexian yaliyo kwenye ulalo wa mawe yenye kuhifadhi maji ya mvua, ambayo yapo kwenye eneo la urithi wa kale lenye ukubwa wa zaidi ya kilomita za mraba 200, katika eneo kame na mazingira magumu, hayo ni mashamba ya matuta ya aina pekee katika eneo la Kaskazini mwa China.

Mtaalamu wa kilimo He Xianlin anasema, “Katika zama za kale, watu walipanga mawe moja baada ya lingine ili kuunda mashamba ya matuta kwenye mteremko wa mlima, Huku wakitumia misingi ya mawe kuhifadhi maji ya mvua yenye thamani kubwa kwa ajili ya umwagiliaji, pamoja na kupanda mimea inayozoea hali ya hewa ya sehemu hiyo, na kutumia kinyesi cha punda kama mbolea asilia, kilimo cha matuta kwenye ardhi kame yanatuwezesha kutumia ardhi na rasilimali yetu chache kwa njia endelevu.”

Mwezi Mei 2022, Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) liliuorodhesha mfumo wa mashamba ya matuta ya Wilaya ya Shexian kwenye eneo kame katika orodha yake ya urithi muhimu wa kilimo duniani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha