

Lugha Nyingine
Mradi unaofadhiliwa na China waboresha usambazaji wa maji katika Mji wa Bafoussam, Cameroon (3)
YAoundE - Kitongoji cha Banengo huko Bafoussam, Mji Mkuu wa Mkoa wa Magharibi wa Cameroon, kilikuwa kinajulikana kwa shida ya uhaba wa maji safi ambapo ubora wa maji katika eneo hilo ulikuwa wa chini, na utokaji wa maji kwenye mabomba haukuwa wa mara kwa mara.
Hali hiyo ngumu katika kitongoji anachoishi Laurence Wandji ilisababisha watoto wake kuamka mapema saa 10:00 Alfajiri ili kuchota maji, wakati mwingine wakitembea kwa umbali mrefu ili kurudi nyumbani na maji. Hali ilikuwa mbaya kiasi kwamba mwanawe, Stones Kaptue, aligundulika kuwa na ugonjwa wa kuhara damu. "Alikaribia kufa," anasema Laurence, ambaye ni mama wa watoto watano.
Paul Djientcheu Leudjeu, Meneja wa Kikanda wa Shirika la Huduma za Maji la Cameroon (CAMWATER) linalomilikiwa na serikali anasema kuwa tatizo la uhaba wa maji lilikuwa baya siyo tu katika Kitongoji cha Banengo bali pia katika Tarafa yote ya Mifi ambako Mji wa Bafoussam unapatikana.
"Kulikuwa na vitongoji fulani ambapo maji yalitoka kwenye mabomba mara moja tu kwa wiki," Leudjeu amesema.
Hata hivyo, mambo yalianza kubadilika na kuwa mazuri wakati Kampuni ya Ujenzi ya China CGCOC ilipowasili Mwaka 2014 na kuanza kujenga mashine za kusafisha maji na vifaa vinavyohusiana na hivyo ambavyo vimeweza kuzalisha maji yenye mita za ujazo 10,000 kila siku. Kampuni hiyo pia ilianza kujenga minara miwili ya matanki ya maji, ambayo ni makubwa zaidi yakiwa na uwezo wa kuhifadhi maji yenye mita za ujazo 1,500. Katika muda wa miaka mitatu, kazi ilikamilika, na kuonesha mwisho wa kipindi cha kwanza cha ujenzi wa mradi unaoungwa mkono na ufadhili wa China.
"Tangu kujengwa kwa mnara mpya wa matanki ya maji, utokaji na usambazaji wa maji umeimarika kwa kiasi kikubwa, tuna matatizo kidogo tu ya maji kwa sasa, tunaweza kusimamia shughuli zetu za kila siku kirahisi zinazohitaji maji, watoto wako salama kwa sasa kwa sababu hawatembei tena umbali mrefu kutafuta maji." amesema mwalimu mmoja mwenye umri wa miaka 41 katika shule ya msingi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma