Walimu wanandoa wanaoshikilia nia ya awali ya kuwa walimu milimani kwa miaka 30

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 24, 2023
Walimu wanandoa wanaoshikilia nia ya awali ya kuwa  walimu milimani  kwa miaka 30
Hii ni picha iliyounganishwa: Huang Yongyong (picha ya juu) na Huang Xiubi (picha ya chini) wakitoa mafunzo darasani katika shule ya msingi ya Nawang ya Wilaya ya Debao mkoani Guangxi. (picha ilipigwa Tarehe 22, Machi)

Shule ya msingi ya Nawang ya Wilaya ya Debao mkoani Guangxi iko katika eneo la milimani. Hivi sasa, wapo wanafunzi 23 katika shule hiyo na walimu wawili tu Huang Yongyong na Huang Xiubi ambao ni wanandoa. Kila siku wanashughulikia kazi mbalimbali zinazohusiana na wanafunzi wao, na ni wikendi tu ndipo wana nafasi ya kurudi nyumbani. Mbali na kutoa mafunzo darasani, pia wanawapikia wanafunzi chakula cha mchana, na usiku wanatakiwa kuwaangalia wanafunzi wanane wanaokaa bwenini.

Mwalimu Huang Yongyong alianza kuwa mwalimu mwaka 1987, na aliwahi kutoa mafunzo katika shule 3, kati yao , alifanya kazi katika shule ya msingi ya Nawang kwa miaka 19. Mwalimu Huang Xiubi alianza kuwa mwalimu mwaka 1993 na amekuwa akifanya kazi katika shule ya msingi ya Nawang kwa miaka 30. Kwa ajili ya wanafunzi watoto hao wa milimani, waliacha mara nyingi fursa ya kuhamishwa hadi mahali pengine wakishikilia kuwa walimu mlimani miaka nenda na miaka rudi, na wamesifiwa na watu wengi kuwa walimu wanandoa wazuri. " Kama watoto wanatuhitaji, tutashikilia kazi yetu siku zote." Huang Yongyong alisema. (Picha na Xinhua/Lu Boan)

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha