Mji wa Luoyang katikati mwa China kuanza tamasha lake la 40 la kitamaduni la maua ya Peony (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 27, 2023
Mji wa Luoyang katikati mwa China kuanza tamasha lake la 40 la kitamaduni la maua ya Peony
Kivutio cha utalii cha Mapango ya Longmen huko Luoyang. (Picha na Idara ya Uenezaji ya Kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ya Manispaa ya Luoyang)

Tamasha la 40 la Kitamaduni la Maua ya Peony la Mji wa Luoyang wa China litafanyika kuanzia tarehe 8 hadi 23, Aprili huko Luoyang, Mkoa wa Henan wa katikati mwa China, likihusisha shughuli kuu 10 na shughuli nyingine 40 za kitamaduni na kitalii zilizopangwa kufanyika kwenye mji huo, imetangaza kamati ya maandalizi ya tamasha hilo tarehe 22, Machi.

Luoyang ulikuwa Mji Mkuu wa enzi 13 za kale za China. Unajulikana kama “mji wa maua ya peony”, ukisifika kwa kuwa na maua mazuri zaidi ya peony katika China.

Hafla ya ufunguzi wa tamasha hilo itafanyika usiku wa tarehe 8, Aprili kwenye uwanja wa kusini wa eneo la kivutio cha utalii la Jengo la kijadi la Peony huko Luoyang, huku kipindi cha kutazama maua hayo kikitazamiwa kuanza tarehe 1, Aprili hadi tarehe 5, Mei.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha