Waziri wa Elimu wa Djibouti asema ushirikiano wa elimu na China unawawezesha vijana wa Djibouti (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 27, 2023
Waziri wa Elimu wa Djibouti asema ushirikiano wa elimu na China unawawezesha vijana wa Djibouti
Mwanafunzi akionyesha kiigaji cha kuendesha gari moshi kwenye Karakana ya Luban ya Djibouti iliyoko Shule ya Viwanda na Biashara ya Djibouti katika Nchi ya Djibouti, Septemba 19, 2022. (Xinhua/Dong Jianghui)

DJIBOUTI CITY - Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wa Djibouti Moustapha Mohamed Mahamoud amesema ushirikiano kati ya nchi yake na China katika sekta ya elimu unaweka msingi imara kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Djibouti.

Akizungumza na mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano ya hivi karibuni, Mahamoud, amesema China na Djibouti zinafurahia ushirikiano wenye "nguvu na mzuri sana" katika sekta mbalimbali za maendeleo.

Mahamoud, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano unaoendelea kukua kati ya nchi hizo mbili katika sekta za elimu, ambao amesema unawawezesha vijana wa nchi hiyo ya Bahari Nyekundu kutumia uwezo wao katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya nchi.

"Tuna ushirikiano imara na mzuri sana kati ya China na Djibouti...China ni moja ya nchi zinazosaidia sana Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya Djibouti katika masuala ya elimu," Mahamoud ameliambia Xinhua.

Waziri huyo amesisitiza kuwa China tayari imeisaidia Djibouti kwa ujenzi wa taasisi mbalimbali za kitaaluma, na kutilia mkazo hasa kujenga vituo vya ubora. Kwa mujibu wake, moja ya vituo hivyo vya ubora vilivyojengwa na China ni Karakana ya Luban nchini Djibouti.

Karakana ya Luban nchini Djibouti ilianzishwa Machi 2019 ikiwa ni ya kwanza ya aina yake katika Bara la Afrika kwa lengo la kutoa mafunzo bora ya ufundi kwa watu wenyeji, haswa vijana wa nchi hiyo.

Waziri huyo pia amesisitiza umuhimu wa kuimarisha zaidi ushirikiano wa China na Djibouti katika sekta ya elimu.

Siku ya Alhamisi, Chuo cha Confucius nchini Djibouti kilizinduliwa katika Mji wa Djibouti, huku wadau wakiahidi kuifanya chuo hicho kuwa jukwaa muhimu la ushirikiano kati ya China na Djibouti.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha