Zambia yawasha rasmi mtambo wa kufua umeme kwa maji uliojengwa na China ili kukabiliana na uhaba wa umeme

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 27, 2023
Zambia yawasha rasmi mtambo wa kufua umeme kwa maji uliojengwa na China ili kukabiliana na uhaba wa umeme
Picha hii iliyopigwa Machi 23, 2023 ikionyesha bwawa katika Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa nishati ya Maji kwenye eneo la chini la mtiririko wa maji ya mto wa Bonde la Kafue katika Mkoa wa Kusini, Zambia. Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amekata utepe kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa kituo hicho cha kuzalisha umeme kwa nishati ya maji kilichojengwa na China, kufuatia kuwashwa kwa jenereta ya tano ya kituo hicho siku ya Ijumaa. (Xinhua)

CHIKANKATA, Zambia - Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amezindua rasmi kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya maji kilichojengwa na China, kufuatia kuwashwa kwa jenereta ya tano ya mashine siku ya Ijumaa.

Jenereta tano katika Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa nishati ya Maji kwenye eneo la chini la mtiririko wa maji ya mto wa Bonde la Kafue kilichojengwa na kampuni ya China ya Sinohydro Corporation, zimeongeza umeme wenye nguvu ya jumla ya megawati 750 kwenye gridi ya taifa ya nchi hiyo.

Huku akieleza kuwa China na Zambia zimekamilisha mradi huo wa kituo cha kuzalisha umeme kwa "njia ya ubunifu," Hichilema amesema mradi huo unaonyesha uhusiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili, na serikali yake imejitolea kukuza zaidi uhusiano na China.

Hichilema ameongeza kuwa kukamilika kwa mradi huo siyo tu jambo zuri kwa sekta ya nishati nchini humo bali pia ni jambo jema kwa uchumi kwa ujumla kwani nishati ni muhimu katika kusukuma uchumi.

Naye Balozi wa China nchini Zambia Du Xiaohui amesema mradi huo ni alama muhimu ya urafiki na ushirikiano kati ya China na Afrika.

Amesema China itaendelea kuchangia ushirikiano wa nyakati zote, wa pande zote na wa hali ya juu na Zambia.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha