Mashindano ya kwanza ya mbio za marathon yafanyika katika Mji wa Suzhou, China, wakimbiaji 25,000 walishiriki (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 27, 2023
Mashindano ya kwanza ya mbio za marathon yafanyika katika Mji wa Suzhou, China, wakimbiaji 25,000 walishiriki
Bingwa wa Mashindano ya Mbio za Marathon ya Suzhou, China kwa wanawake Yang Hua akivuka mstari wa kumalizia kwenye Uwanja wa Kituo cha Michezo cha Olimpiki cha Suzhou, katika Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China. (Picha imetolewa na kamati ya maandalizi ya Mbio za Marathon za Suzhou)

Mashindano ya kwanza ya mji ya mbio za marathon ya Suzhou, yamefanyika siku ya Jumapili kwenye kando ya Ziwa Jinji katika Mji wa Suzhou wa Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China.

Kaulimbiu ya mashindano hayo ya mbio za marathon kwa mwaka huu ni "zaidi ya hayo", ambapo zimehusisha mbio za aina tatu ambazo ni: mbio za marathon kamili, nusu mbio za marathon, na mbio za kifamilia, na jumla ya wakimbiaji 25,000 walishiriki katika mashindano ya mbio zote hizo.

Katika mashindano ya mbio za marathon kwa wanaume, mshiriki Guan Yousheng alishinda nafasi ya kwanza kwa kukimbia kwa saa 2, dakika 15 na sekunde 41. Katika mbio za marathon kwa wanawake, mshiriki Yang Hua alishinda ubingwa kwa kukimbia kwa muda wa saa 2, dakika 38 na sekunde 18.

Mshiriki Qi Zhenfei alishinda nafasi ya kwanza kwenye nusu ya mbio za marathon kwa wanaume kwa kukimbia kwa muda wa saa 1, dakika 6 na sekunde 38. Diriba Chaltu Dida kutoka Ethiopia alishinda nusu ya mbio za marathon kwa wanawake kwa kukimbia kwa muda wa saa 1, dakika 16 na sekunde 7.

Mashindano hayo ya mbio za Marathon ya Suzhou kwa Mwaka 2023 yametilia maanani kikamilifu uendeshaji wa kidijitali wa tukio husika, kuweka kipaumbele cha juu katika jukwaa la huduma jumuishi linalotumia teknolojia za akili bandia, na kuweka kituo kikuu cha teknolojia ya 5G kwenye eneo la mbio hizo.

Kupitia Mtandao wa Mambo na teknolojia ya data kubwa, mashindano ya mbio hizo yametambua hakikisho la ushiriki wa wakimbiaji, usimamizi wa matukio, kuonyesha kwa jumla maelekezo na uratibu wa tukio zima, na kuboresha kiwango cha mashindano . 

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha