Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Kijiji cha Taipan cha China yavutia watu wengi (9)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 28, 2023
Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Kijiji cha Taipan cha China yavutia watu wengi
Mtazamaji akipiga ngoma kando ya uwanja ili kuwatia moyo wachezaji.

Jioni ya tarehe 26, Machi, fainali za ligi ya kwanza ya mpira wa kikapu ya “Vijiji Vizuri” ya Mkoa wa Guizhou, China zilianza kwenye Kijiji cha Taipan cha Wilaya ya Taijiang ya Eneo linalojiendesha la Makabila ya Wamiao na Wadong la Qiandongnan. Michezo hiyo imevutia watazamaji wengi na kuleta hali motomoto.

Awali ligi hiyo ya mchezo wa mpira wa kikapu katika Kijiji cha Taipan ni shughuli ya mashindano ya Mchezo wa mpira wa kikapu katika siku ya kuonja mazao mapya ya kijiji hicho. Katika ligi hiyo, wachezaji hutoka makabila mbalimbali yanayokaa kwenye sehemu hiyo. Mwelezaji wa mashindano hayo katika ligi hiyo hutumia lugha sanifu ya Kichina na lahaja ya kikabila kueleza hali ya mashindano. Wasanii washangiliaji hucheza ngoma na kuimba nyimbo za kikabila wakati wa mapumziko. Tuzo za washindi katika ligi hiyo huwa ni ng’ombe, nguruwe, na tikitimaji……Ligi hiyo ya kipekee ya Kijiji cha Taipan imevutia watu wengi tangu imekuwa maarufu kwenye mtandao wa intaneti wa China mwaka 2022. Wachina huiita “Ligi ya Shirikisho la Michezo ya Mpira wa Kikapu la Vijiji (Vijiji BA)”. Hivi sasa timu zinazoshiriki kwenye ligi hiyo zimeongezeka zikiwemo timu za vijiji na vitongoji vya jirani za hapo awali pamoja na timu za wilaya mbalimbali za Eneo zima la Qiandongnan katika Mkoa wa Guizhou wa China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha