Shughuli mfululizo za Msimu wa Utalii wa Wilaya ya Hongtong ya China zaanza

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 30, 2023
Shughuli mfululizo za Msimu wa Utalii wa Wilaya ya Hongtong ya China zaanza

Tarehe 29, Machi, mkutano wa kutangaza shughuli mfululizo za Msimu wa Utalii wa Wilaya ya Hongtong ya Mji wa Linfen mkoani Shanxi, China ulifanyika hapa Beijing. Imeelezwa kuwa, shughuli hizo zitafanyika kuanzia tarehe 29, Machi hadi tarehe 1, Mei, na zitahusisha mjadala wa utamaduni wa kienyeji, maonyesho ya maandiko ya kaligrafia ya Kichina na picha za kuchorwa, maonesho ya picha za kupigwa, siku ya vyakula vitamu, na maonesho ya opera za kienyeji za China. Licha ya hayo, kutakuwa na shughuli nyingine za mikutano ya kuvuta uwekezaji, kufanya makongamano, na mikutano ya kutangaza utalii.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha