Pande mbili za China na Vietnam zafanya semina ya 17 ya nadharia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 30, 2023
Pande mbili za China na Vietnam zafanya semina ya 17 ya nadharia
Li Shulei, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya CPC, na Nguyen Xuan Thang, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV), Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Nadharia na Mkuu wa Chuo cha Kitaifa cha Siasa cha Ho Chi Minh, wakihudhuria semina ya 17 ya nadharia ya pande hizo mbili kupitia njia ya video, Machi 29, 2023. Pande hizo mbili zimefanya semina yao ya 17 ya nadharia siku ya Jumatano kupitia njia ya mtandao, ili kubadilishana uzoefu uliopatikana katika ukuzaji wa mbinu mpya za usimamizi wa kijamii katika zama za upashanaji wa habari. (Xinhua/Zhai Jianlan)

BEIJING - Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) vimefanya semina yao ya nadharia ya 17 siku ya Jumatano kupitia njia ya mtandao, vikibadilishana uzoefu uliopatikana katika ukuzaji wa mbinu mpya za usimamizi wa kijamii katika zama za upashanaji wa habari.

Li Shulei, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na Mkuu wa Idara ya Uenezi wa Kamati Kuu ya CPC, amehudhuria semina hiyo.

Li amesema kuwa maafikiano yaliyofikiwa na viongozi wa pande zote mbili yalitoa muongozo kwa ajili ya kuimarisha uhusiano kati ya pande hizo mbili na nchi hizo mbili, pamoja na kuhimiza lengo la ujamaa kwa pande zote mbili.

“Kutokana na mtazamo wa kimkakati wa kuendeleza ustawishaji wa Taifa la China katika sekta zote kupitia njia ya maendeleo ya kisasa ya China, Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC uliofanyika Mwezi Oktoba mwaka jana ulitoa mwelekeo mpya ya kuboresha mfumo wa utawala wa kijamii,” Li amesema.

Huku akieleza kuwa China ina nia ya kuweka maslahi ya watu kwenye kipaumbele cha juu, Li amesema ili kuboresha usimamizi wa kijamii kwa njia ya upashanaji wa habari, nchi hiyo imeweka kithabiti wazo la kutawala nchi kwa mujibu wa sheria, kusisitiza matumizi ya teknolojia mpya na namna ya kuzitumia, na kutekeleza kikamilifu jukumu la mtandao wa intaneti katika kueneza utamaduni wa kimaendeleo na mtazamo wa maadili makuu.

Kwa upande wake Nguyen Xuan Thang, ambaye ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPV, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Nadharia na Mkuu wa Chuo cha Kitaifa cha Siasa cha Ho Chi Minh, amesifu mafanikio ya China katika kuimarisha na kuendeleza mbinu mpya za usimamizi wa kijamii, huku akieleza nia ya kuendeleza urafiki wa jadi na kuimarisha hali ya kuaminiana kati ya pande hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha