Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya kivuko nchini Ufilipino yafikia 29

(CRI Online) Machi 31, 2023
Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya kivuko nchini Ufilipino yafikia 29
(Picha kutoka Xinhua)

Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya moto iliyotokea kwenye kivuko cha baharini karibu na Jimbo la Basilan Kusini nchini Ufilipino, imezidi watu 29.

Kikosi cha Ulinzi wa Pwani nchini humo kimesema, watu 230 waliokuwa kwenye kivuko hicho wameokolewa. Vikosi vya Utafutaji na uokoaji vimefanikiwa kupata miili 18 kwenye kivuko, na watu wengine 11 walifariki kwenye maji walipojirusha baharini kukwepa moto huo.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha