Kituo cha huduma kwa watoto wenye mahitaji maalum chaleta matumaini kwa watoto wenye tatizo la Usonji

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 03, 2023
Kituo cha huduma kwa watoto wenye mahitaji maalum chaleta matumaini kwa watoto wenye tatizo la Usonji
Cheng Zhifang (wa katikati) akimfundisha mtoto mwenye tatizo la usonji kufanya mazoezi ya utambuzi kwenye kituo cha huduma kwa watoto wenye mahitaji maalum cha Starlight mjini Xining, Mkoa wa Qinghai wa Kaskazini Magharibi mwa China tarehe 30, Machi, 2023.

Chen Zhifang ni mwanzilishi  wa Kituo cha huduma kwa watoto wenye mahitaji maalumu cha Starlight cha Mji wa Xining. Kikiwa kilianzishwa mwaka 2015, kituo hicho cha huduma ni shirika lisilo la faida la umma linalotoa mazoezi ya uponeshaji na uingiliaji kati wa kipindi cha mapema kwa watoto wenye tatizo la usonji, ulemavu wa akili na ulemavu wa kuongea kwa ufasaha. Hivi sasa watoto 132 wenye  tatizo la usonji wanapokea mazoezi mbalimbali ya uponyaji kwenye kituo hicho.

Katika miaka minane iliyopita, kituo hicho kimekuwa sehemu ya kuleta matumaini kwa watoto wengi wenye tatizo la usonji na wanafamilia wao.

Kituo hicho hutoa mbinu za kutoa mafunzo mbalimbali tofauti kutokana na uwezo wa utambuzi, kujieleza na uwezo wa kimwili wa kila mtoto. Kwa sasa watoto wengi wa kituo hicho wanaweza kwenda kwenye maduka, kupanda mabasi hata kurudi shuleni.

“Nikiwa mzazi wa mtoto mwenye tatizo la usonji, ninatumai kuwaambia watu wengine wengi kuhusu uzoefu wangu katika mazoezi ya uponyeshaji wa mtoto wangu, ili kuwasaidia watoto wengi zaidi wenye tatizo la usonji wajiunge na jamii” anasema Chen. (Xinhua/Zhang Long)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha