Mashindano ya Mbio za kuvuka mbuga na mapori za AMOY50 na Mashindano ya kutembea ya kujenga afya ya Umma ya Mji wa Xiamen yaanza

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 10, 2023
Mashindano ya Mbio za kuvuka mbuga na mapori za AMOY50 na Mashindano ya kutembea ya kujenga afya ya Umma ya Mji wa Xiamen yaanza

Asubuhi ya tarehe 9, mwezi huu, Mashindano ya Mbio za kuvuka mbuga na mapori za AMOY50 2023 za Mji wa Xiamen, pamoja na mashindano ya kutembea ya kujenga afya ya umma yote ya mji huo yameanza huko Xiamen, China. Wakimbiaji na watembeaji zaidi ya 2000 wameshiriki kwenye mashindano hayo, wakiwemo wachezaji kutoka maeneo ya Taiwan, Hong Kong na Macao.

Njia iliyopangwa ya mashindano hayo iko kwenye “Njia ya mbio ya Milima Bahari ya Kilomita 50” huko Xiamen, ikionyesha vizuri mandhari ya mazingira asilia ya Mji wa Xiamen. Shughuli hiyo imechukua muundo wa kuunganisha mashindano ya kutembea na mbio za kuvuka mbuga na mapori, ambazo zimevutia washiriki wengi zaidi.

Siku hiyo, Tamasha la Michezo la Siming 2023 pia limefunguliwa huko Xiamen, China. Inafahamika kuwa, tamasha hilo lilianzishwa Mwaka 2018, na limevutia washiriki karibu 280,000 hivi kutoka nchi na maeneo zaidi ya 60, miongoni mwao kuna watu zaidi ya 10,000 kutoka eneo la Taiwan waliopo kwenye Xiamen. Tamasha hilo la mwaka huu litaendelea hadi Mwezi Agosti, na litafanya shughuli tano kuu, kama vile mashindano ya kupanda baiskeli barabarani, michezo ya ndondi n.k..

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha