Kampuni ya Magari ya Tesla kujenga kiwanda kipya kikubwa cha kuzalisha bidhaa za Megapack huko Shanghai, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 10, 2023
Kampuni ya Magari ya Tesla kujenga kiwanda kipya kikubwa cha kuzalisha bidhaa za Megapack huko Shanghai, China
Picha hii iliyopigwa Tarehe 9 Aprili 2023 ikionyesha hafla ya kusainiwa kwa makubaliano kuhusu mradi wa kiwanda kikubwa cha Kampuni ya Magari ya Tesla cha Shanghai iliyofanyika Shanghai, Mashariki mwa China. (Xinhua/Ding Ting)

SHANGHAI - Kampuni ya kuunda magari ya Marekani, Tesla Inc. Jumapili imetangaza kwamba itajenga kiwanda kikubwa kipya huko Shanghai, ambacho kitatengeneza bidhaa za kampuni hiyo ya Betrii za Megapack zinazohifadhi nishati.

Kiwanda hicho kipya kimepangwa kuanza kujengwa katika robo ya tatu ya mwaka huu na kuanza rasmi uzalishaji katika robo ya pili ya Mwaka 2024, Kampuni ya Tesla imesema katika hafla ya kutia saini mradi huo huko Shanghai.

Kiwanda hicho kitazalisha betrii za Megapack zenye watts 10,000 kila mwaka, sawa na takriban umeme wa kuhifadhiwa wenye nguvu ya GWh 40. Bidhaa hizo zitauzwa duniani kote.

Megapack ni betri yenye nguvu ambayo hutoa uhifadhi na usaidizi wa nishati, kusaidia kuleta utulivu wa gridi ya taifa na kuzuia kukatika kwa umeme, maelezo kwenye tovuti ya Kampuni ya Tesla yanaonyesha.

Kiwanda hicho kipya cha kampuni hiyo kitapatikana katika Eneo Maalum la Lin-gang la Eneo la Majaribio la Biashara Huria la China (Shanghai).

Zhuang Mudi, Naibu Katibu Mkuu wa Serikali ya Manispaa ya Shanghai, amesema mradi huo utasaidia kusukuma maendeleo ya tasnia mpya ya kuhifadhi nishati, pamoja na mageuzi ya kijani na utoaji hewa kidogo ya kaboni ya Shanghai.

Januari 2019, Kampuni ya Tesla ilifungua rasmi kiwanda chake cha kiotomatiki cha kuunda magari yanayotumia betrii, Gigafactory cha Shanghai, na kuwa kampuni ya kwanza kufaidika na sera mpya inayowaruhusu watengenezaji magari wa kigeni kuanzisha kampuni tanzu zinazomilikiwa nao kabisa nchini China.

Hiki ni kiwanda cha kwanza cha kiotomatiki cha kuunda magari, Gigafactory cha Kampuni ya Tesla nje ya Marekani, na kiwanda hicho kilizalisha magari 710,000 katika Mwaka 2022, ikiwa ni ongezeko la asilimia 48 kutoka kiwango cha Mwaka 2021.

China imekuwa ikisisitiza dhamira yake ya kufungua mlango katika wiki za hivi karibuni katika hafla tofauti, ikionyesha utayari wake wa kunufaika pamoja na faida za soko kubwa la matumizi la Dunia, na kushikilia nia yake ya tangu mwanzo mpaka mwisho katika kuhimiza maendeleo ya pamoja ya nchi mbalimbali.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha