Ustawishaji mahiri wa vijiji watajwa kuwa chanzo cha harusi za kuvutia za Kabila la Watajiki huko Xinjiang, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 10, 2023
Ustawishaji mahiri wa vijiji watajwa kuwa chanzo cha harusi za kuvutia za Kabila la Watajiki huko Xinjiang, China
Marmathan Tirmur akimsaidia bibi harusi wake Gulihan Zabibili kupanga mapambo kwenye mikono yake kwenye nyumba yao mpya iliyoko Wilaya inayojiendesha ya Kabila la Watajik ya Taxkorgan, katika Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang, China, Machi 20, 2023. (Xinhua/Hu Huhu)

URUMQI - "Harusi yenye furaha!" Shangwe nyingi zililipuka kwenye sherehe ya harusi iliyopambwa kwa kufuata mila na desturi za kabila wa Watajiki, ambapo Gulihan Zangabili alifunga pingu za maisha na mpenzi wake.

Tukio hilo zuri na la kufurahisha lililodumu kwa siku tatu katika Kijiji cha Fumin lilileta nguvu na furaha kwa wanakijiji wanaoishi kwenye Uwanda wa Pamir, Magharibi ya mbali ya Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang, Kaskazini Magharibi mwa China.

Kwa bibi harusi mwenye umri wa miaka 25 wa kabila la Watajik na bwana harusi Marmathan Tirmur, waliopendana zaidi ya miaka mitatu iliyopita, sherehe ya harusi ya jadi ilikuwa kwenye orodha yao ya mambo ya kufanya.

"Sasa viwango vyetu vya maisha vinaturuhusu kuchagua njia nyingi za kufanya harusi yetu, lakini bado tunapendelea kufanya hivyo kwa sherehe za jadi kutokana na mila na desturi zetu ,” amesema bwana harusi.

Zikiwa zimeorodheshwa kwenye orodha ya kitaifa ya urithi wa utamaduni usioshikika wa China Mwaka 2008, taratibu za kijadi za harusi za Kabila la Watajiki zinadumisha mila za kipekee na kila mara huchukuliwa kama sherehe za muziki, dansi na chakula ili kuwaonyesha wachumba wapya kwa kutumia ndoa yao ya kifahari.

Kwa mujibu wa takwimu za ofisi ya ustawishaji vijiji ya eneo hilo, serikali ya mtaa Mwaka 2017 ilianza kutekeleza mradi wa uhamishaji wakazi wa Tatikuli, ukisaidia wakulima na wafugaji zaidi ya 1,400 katika vitongoji vitano vya wilaya hiyo kuhamia nyumba mpya karibu na makazi ya wilaya kutoka maeneo ya mbali ya milima.

"Kwa sababu ya kuendelea kwa kazi ya ustawishaji vijiji, ubora wa maisha ya wanakijiji umeboreshwa sana ikilinganishwa na hapo awali," Elken Yusain, mkuu wa ofisi hiyo amesema.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha