Pilikapilika za kuchuma mazao kwenye “kiwanda cha Nyanya” cha Neijiang, Mkoa wa Sichuan, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 11, 2023
Pilikapilika za kuchuma mazao kwenye “kiwanda cha Nyanya” cha Neijiang, Mkoa wa Sichuan, China
Mfanyakazi akichuma nyanya kwenye banda la kijani la kisasa katika Bustani ya Kilimo cha Kisasa iliyopo Mji Mdogo wa Yinshan, Wilaya ya Zizhong, Mji wa Neijiang, Mkoa wa Sichuan, nchini China, Tarehe 10, Aprili.

Hivi sasa, zaidi ya mimea 40,000 ya nyanya iliyopandwa katika Bustani ya Kilimo cha Kisasa ya Mji Mdogo wa Yinshan, Wilaya ya Zizhong, Mji wa Neijiang, Mkoa wa Sichuan nchini China inakaribia kipindi cha kuchuma nyanya. Wafanyakazi wana pilika za kufanya kazi ya kuchuma nyanya, kuzihamisha, kuzipanga katika madaraja, kuzifungisha na kuzisambaza sokoni.

Katika miaka ya hivi karibuni, Mji wa Neijiang, Mkoa wa Sichuan umeendeleza kilimo kinachotumia vifaa vya teknolojia za hali ya juu kwa nguvu, kama vile kutumia teknolojia za kisasa kudhibiti hali ya joto na kilimo kisichotumia udongo kwa uzalishaji wa kilimo, kukuza ufanisi wa kilimo, kuongeza mapato ya wakulima, na kusaidia ustawishaji wa vijiji. (Picha na vip.people.com.cn)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha