Rais Xi Jinping akagua Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 12, 2023
Rais Xi Jinping akagua Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitembelea kituo cha ufugaji wa samaki na mazao ya majini katika Mji wa Zhanjiang, Mkoa wa Guangdong, Aprili 10, 2023. Rais Xi Jumatatu amekagua Mkoa wa Guangdong, China. (Xinhua/Ju Peng)

GUANGZHOU - Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, Jumatatu amekagua Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China.

Kwanza alienda katika Mji wa Zhanjiang, ambako alitembelea kituo cha kilimo cha majini, eneo la misitu ya mikoko, bandari, na mradi wa ugawaji wa rasilimali za maji.

Rais Xi amefahamishwa kuhusu jitihada za kuendeleza ufugaji wa samaki, uhifadhi na ukuzaji wa mazao ya majini, kuimarisha ulinzi wa misitu ya mikoko, kuongeza muunganisho wa miundombinu ya usafiri, kuendeleza maendeleo shirikishi ya Guangdong na mkoa wa jirani wa kisiwa wa Hainan, na kuboresha ugawaji wa rasilimali za maji. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha