IMF yakadiria ongezeko la 5.2% la uchumi wa China Mwaka 2023 na kuwa "mchangiaji muhimu " kwa ukuaji wa uchumi wa Dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 12, 2023
IMF yakadiria ongezeko la 5.2% la uchumi wa China Mwaka 2023 na kuwa
Watembea kwa miguu wakipita karibu na makao makuu ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) huko Washington, D.C., Marekani, Aprili 10, 2023. (Xinhua/Liu Jie)

WASHINGTON - Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Jumanne wiki hii limekadiria kuwa ongezeko la uchumi wa China litafikia asilimia 5.2 Mwaka 2023 na kufikia asilimia 4.5 Mwaka 2024.

"Tunakadiria (kwa China) ongezeko la uchumi wa China litafikia asilimia 5.2 Mwaka 2023. Hiyo ni kutoka asilimia 3 mwaka jana," Pierre-Olivier Gourinchas, Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti wa IMF, ameuambia mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumanne juu ya ripoti ya mtazamo wa hivi punde wa Uchumi wa Dunia (WEO).

Gourinchas amesema, kwa kuzingatia ukubwa wa uchumi wa China, kwa kiwango hicho itakuwa mchangiaji muhimu wa ongezeko la uchumi wa Dunia katika mwaka ujao, na "ni moja ya (sehemu) ya habari kubwa za Mwaka 2023" kwamba uchumi wa China unaonekana kufunguliwa kwa kasi na kuimarika kwa nguvu.

"Mawimbi ya UVIKO-19 yalipopungua (nchini China) Mwezi Januari mwaka huu, mzunguko wa uchumi wa hali ya kawaida, na viashiria vya uchumi vya kiwango cha juu, kama vile mauzo ya bidhaa kwa rejareja na manunuzi ya tiketi za kusafiri, vilianza kuongezeka," IMF imesema katika ripoti yake hiyo.

"Kufunguliwa tena na kukua kwa uchumi wake kunaweza kuleta maendeleo yenye hamasa , na kuleta matunda zaidi ya kiuchumi kwa nchi zilizo na uhusiano mkubwa wa kibiashara na kutegemea utalii wa China," inaongeza ripoti hiyo.

Kwa mujibu wa makadirio ya IMF, ongezeko la uchumi wa Dunia litafikia asilimia 2.8 Mwaka 2023, ikiwa ni asilimia 0.1 chini ya makadrio yake ya mwezi Januari.

Ongezeko la uchumi wa Dunia linakadiriwa kuwa asilimia 3.4 Mwaka 2022, kushuka hadi asilimia 2.8 Mwaka 2023, na kupanda hadi asilimia 3 Mwaka 2024, imeongeza ripoti hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha