Njia mpya ya  usafiri wa ndege za mizigo kati ya China na Ubelgiji yahimiza usambazaji wa bidhaa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 12, 2023
Njia mpya ya  usafiri wa ndege za mizigo kati ya China na Ubelgiji yahimiza usambazaji wa bidhaa
Wafanyakazi wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya ndege ya mizigo ya Shirika la Ndege la SF kusherehekea uanzishwaji wa njia ya usafiri wa ndege za mizigo inayounganisha Mji wa Qingdao nchini China na Mji wa Liege nchini Ubelgiji, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Qingdao Jiaodong mkoani Shandong, Mashariki mwa China, Aprili 11, 2023. (Shirika la Ndege la SF/ Xinhua)

BEIJING - Shirika la Ndege la SF limesema, Njia ya usafiri wa ndege za mizigo inayounganisha Mji wa Qingdao, Mashariki mwa China na Mji wa Liege wa Ubelgiji imeanzishwa rasmi siku ya Jumanne, na kuongeza njia mpya ya usambazaji wa mizigo kati ya China na Ulaya.

Ndege mbili za mizigo zitakazofanya usafiri wa kwenda na kurudi zimepangwa kuendeshwa kati ya China na Ulaya kila wiki kwenye njia hii, na kuongeza uwezo wa kusambaza vifurushi vya tani 400 , shirika hilo la ndege za mizigo limesema.

Kabla ya kufunguliwa kwa njia hii mpya, Tarehe 1 Aprili shirika hilo la ndege lilianzisha njia ya usafiri wa ndege za mizigo inayounganisha Mji wa Ezhou wa Mkoa wa Hubei, katikati mwa China, na Mji wa Liege nchini Ubelgiji.

Shirika la Ndege la SF ni tawi la usafiri wa anga la kampuni inayoongoza nchini China ya usafirishaji wa mizigo ya SF Express. Ni kampuni kubwa zaidi ya kusafirisha mizigo kwa njia ya anga nchini China inayoendesha ndege za mizigo zaidi ya 80.

Kampuni hiyo imeanzisha mtandao wa njia za ndege za mizigo zinazofika kote nchini China, kutoa huduma barani Asia, na kufika Ulaya na Marekani. Imejitolea kuendelea kupanua ukubwa wa shehena za mizigo inazobeba na kuimarisha uwezo wa huduma ya usambazaji wa vifurushi kwa ndege za mizigo ili kukuza maendeleo yenye ubora wa juu.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha