IMF yataka kupitishwa sera kali ya fedha kusaidia kudhibiti mfumuko wa bei

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 13, 2023
IMF yataka kupitishwa sera kali ya fedha kusaidia kudhibiti mfumuko wa bei
Vitor Gaspar, Mkurugenzi wa Idara ya Masuala ya Fedha wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Washington, D.C., Marekani, Aprili 12, 2023. (Xinhua/Liu Jie)

WASHINGTON - Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Jumatano limehimiza watunga sera za fedha kupitisha sera kali za kifedha ili kusaidia benki kuu za nchi na maeneo mbalimbali kupambana na mfumuko wa bei.

"Huku kukiwa na mfumuko mkubwa wa bei, mazingira makali ya kifedha, na kuongezeka kwa deni, watunga sera wanapaswa kuweka kipaumbele katika kuweka sera ya fedha zinazoendana na sera za benki kuu ili kuhimiza utulivu wa bei na mambo ya fedha," IMF imesema katika ripoti yake iliyochapishwa kwenye wavuti wakati ilipotoa ripoti yake mpya ya Ufuatiliaji wa mambo ya utawala ya kifedha.

Ripoti hiyo imesema kuwa nchi nyingi zitahitaji msimamo mkali wa kifedha kusaidia mchakato unaoendelea wa kutokomeza mfumko wa bei -- haswa ikiwa mfumuko wa bei utaendelea kudumu zaidi.

"Sera kali ya fedha itaruhusu benki kuu kuongeza viwango vya riba kwa alama za chini, hali ambayo itasaidia kudhibiti gharama za kukopa kwa serikali na kudhibiti udhaifu wa mambo ya fedha," imesema ripoti hiyo ya kwenye wavuti, iliyoandikwa na mwanauchumi wa IMF Francesca Caselli na wenzake.

Wakati huo huo, IMF imebainisha kuwa sera kali za kifedha zinahitaji "njia bora zaidi za usalama zinazolengwa kulinda familia zenye hali dhaifu zaidi," ikiwa ni pamoja na kushughulikia hali ya ukosefu wa usalama wa chakula, huku zikiwa na ukuaji wa jumla wa matumizi.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha