Maelfu ya watu washerehekea Siku ya Kumwagiana Maji katika Mji wa Mangshi, mkoani Yunnan, Kusini Magharibi mwa China (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 14, 2023
Maelfu ya watu washerehekea Siku ya Kumwagiana Maji katika Mji wa Mangshi, mkoani Yunnan, Kusini Magharibi mwa China
Makumi kwa maelfu ya watu wa makabila mbalimbali wakikusanyika pamoja kwenye uwanja wa Mji wa Mangshi na kusherehekea kwa furaha Siku ya Kumwagiana Maji yenye hali motomoto. (Picha na JiaoDi)

Tarehe 12, Aprili, Bustani ya Kuburudika ya Mangshi, mkoani Yunnan ilijaa watu wengi na ilikuwa yenye hali motomoto. Makumi kwa maelfu ya watu wa makabila mbalimbali waliovalia mavazi mazuri ya sikukuu walipiga ngoma za kikabila, kucheza dansi za kijadi, kumwagiana maji na kutakiana heri na baraka ili kusherehekea pamoja kwa furaha siku hiyo ya kumwagiana maji.

Inafahamika kwamba Siku ya Kumwagiana Maji ni siku ya jadi yenye sherehe kubwa zaidi katika mwaka kwa watu wa Kabila la Wadai. Mwaka 2006, sherehe za siku hiyo ya jadi ziliwekwa kwenye orodha ya kwanza ya urithi wa utamaduni usioshikika katika ngazi ya kitaifa.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha