Katika Picha: Furahia maua ya Peony yanayochanua huko Luoyang, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 17, 2023
Katika Picha: Furahia maua ya Peony yanayochanua huko Luoyang, China
Picha iliyopigwa Tarehe 10, Aprili, 2023 ikionesha ua la Peony linalochanua kwenye Bustani ya Kitaifa ya Maua ya Peony huko Luoyang, Mkoa wa Henan wa katikati ya China. (People’s Daily Online/Du Mingming)

Majira ya mchipuko yanatambuliwa kuwa wakati mzuri zaidi wa kutembelea Mji wa Luoyang wa Mkoa wa Henan wa katikati ya China, kwa kuwa maua ya Peony ya mji huo yameingia kipindi chake cha kuchanua zaidi, yakivutia watalii wengi kutoka ndani ya China na nchi nyingine mbalimbali.

Maua ya Peony huashiria utajiri, baraka na ustawi katika China. Huchukuliwa kuwa maua ya hadhi ya juu zaidi ya mapambo, na yamepewa jina la “Mfalme wa Maua”. Mji wa Luoyang ukiwa ni mji wa kifalme wa enzi zaidi ya 13 katika historia ya China, una historia ya zaidi ya miaka 1600 katika upandaji maua ya peony na unajisifia kuwa na maua mazuri zaidi ya Peony kuliko maeneo yote nchini China.

Ili kuthamini maua hayo mazuri, mji huo umekuwa ukifanya tamasha la kitamaduni la maua ya peony kila mwaka kuanzia 1983. Mnamo Mwaka 2010, tamasha hilo liliongezwa kwenye orodha ya urithi wa utamaduni usioshikika wa kitaifa wa China, na kupandishwa hadhi yake na kuwa shughuli ya kitamaduni ya kitaifa.

Tamasha la 40 la Kitamaduni la Maua ya Peony la Luoyang, China linaloendelea litafanyika hadi Tarehe 23, Aprili, na kipindi cha kutazama maua kitaendelea hadi Tarehe 5, Mei.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha