Michezo yawa kadi mpya ya maendeleo ya mji wa Wuhan (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 17, 2023
Michezo yawa kadi mpya ya maendeleo ya mji wa Wuhan
Maonyesho ya Bidhaa za Matumizi za Michezo ya Wuhan 2023. (Picha na Zhang Pei/Tovuti ya Gazeti la Umma)

Saa 1:30 asubuhi mnamo Aprili 16, mashindano ya mbio za Marathon ya Wuhan, ambayo yalianzishwa tena kwa wakati baada ya miaka mitatu.

Siyo tu mbio za marathon, katika miaka ya hivi karibuni, Wuhan imeandaa mashindano ya michezo ya kiwango cha juu zaidi ya 100. Ili kuhimiza maendeleo ya michezo na kuongoza wimbi la watu wote kufanya mazoezi ya kujenga mwili, Wuhan inaharakisha maendeleo ya michezo ya kiwango cha juu.

Maonyesho ya Bidhaa za Matumizi za Michezo ya Wuhan 2023 yanaangazia lengo la "kuendeleza michezo, kuhimiza matumizi, na kuchangia uchumi", yakivutia jumla ya kampuni 140 hivi za kuendesha shughuli za michezo na vifaa vya michezo kushiriki katika maonyesho hayo, kuwezesha watumiaji wa bidhaa za michezo, chapa za bidhaa, na masoko ya bidhaa kuwasiliana ana kwa ana kwa pamoja.

Takwimu zinaonyesha kuwa watu wa Wuhan wanaoshiriki kwenye michezo mara kwa mara katika mazoezi ya kujenga viungo wamefikia 49.64%, sampuli za wanaofikia kiwango cha utimamu wa afya ya mwili kwa wakaazi zinafikia 92.53%, wastani wa utumiaji wa eneo la uwanja wa michezo kwa kila mtu unafikia mita za mraba 2.45, na kuna shughuli za mazoezi ya kujenga mwili zipatazo 1,200 kwa mwaka mzima.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha