Shughuli ya kuonja Chai ya Vine ya Zhangjiajie, China yafanyika Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 19, 2023

Sehemu ya kufanya mahojiano na wageni. (Picha na waandaaji wa shughuli)

Sehemu ya kufanya mahojiano na wageni. (Picha na waandaaji wa shughuli)

Tarehe 18, Aprili, Shughuli ya Kuonja Chai ya Vine ya Zhangjiajie, katika Mkoa wa Hunan wa China ilifanyika katika Jengo Jipya la Vyombo vya Habari la Shirika la Habari la People's Daily, hapa Beijing.

Kaulimbiu ya shughuli hiyo ni "Acha Dunia itambue Chai ya Vine na acha Chai ya Vine iende duniani" na iko chini ya mwongozo wa Serikali ya Mji wa Zhangjiajie, kuandaliwa na Serikali ya Eneo la Yongding katika Mji wa Zhangjiajie, kuratibiwa na kuratibiwa kwa pamoja na Ofisi ya Kilimo na Vijiji ya Eneo la Yongding na Idara ya Uenezi ya Kamati ya Chama ya Eneo la Yongding. Shughuli mbalimbali zilizofanyika sambamba na shughuli kuu hiyo ilikuwa ni pamoja na maonyesho ya kitamaduni, hotuba za wageni, maonyesho ya bidhaa za Chai ya Vine, utiaji saini wa mradi wa ushirikiano na mahojiano ya mezani, na kadhalika.

Mji wa Zhanjiajie wa Mkoa wa Hunan una mandhari nzuri sana, pia unazalisha chai ya vine ambayo ni yenye ubora wa juu ya Hunan. Chai ya Vine inakua katika Milima ya Wuling, ambayo pia inajulikana kama chai ya mzabibu wa majani madogo. Kutokana na kuwa na mseto wa flavonoids katika mimea yake, inajulikana kama "mfalme wa flavonoids". Ina kazi nyingi kama vile kusafisha koo na kulinda ini.

Kama eneo kuu la uzalishaji wa chai ya vine, Eneo la Yongding ya Mji wa Zhangjiajie lina jina la "Mji wa Chai ya Vine ya China". Katika miaka ya hivi karibuni, eneo hilo limezingatia kipaumbele cha ikolojia, na usimamizi wa chapa, na kuendelea kuhimiza mageuzi na uboreshaji wa tasnia ya chai ya vine, na kugeuza "kipande kidogo cha chai" kuwa "tasnia kubwa", ili harufu ya kuvutia ya chai ya Hunan iweze kusafiri maelfu ya maili hadi duniani.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha