Picha za maua ya peony zilizochorwa huko Pingle zaonesha hali mpya ya ustawishaji wa vijiji

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 20, 2023
Picha za maua ya peony zilizochorwa huko Pingle zaonesha hali mpya ya ustawishaji wa vijiji
Mchoraji akichora picha ya maua ya peony kwenye kipepeo cha kijadi cha China katika Kijiji cha Pingle Aprili 11, 2023. (Picha na Mwandishi wa People's Daily Online, Du Mingming)

"Maua" yana nguvu kiasi gani? Kundi la wachoraji wakulima wanaotegemea kazi ya kuchora picha za maua ya peony wanaweza kupata mapato ya zaidi ya yuan milioni 100 ( sawa na dola Milioni 15 hivi za Kimarekani) kwa mwaka kwa ajili ya kijiji chao.

Wanakijiji wa Eneo la Makazi la Pingle (zamani Kijiji cha Pingle) la mji wa Wilaya ya Pingle katika Eneo la Mengjin la Mji wa Luoyang, Mkoa wa Henan, hubeba majembe kwenda mashambani wakati kilimo kinapokuwa na shughuli nyingi, na wakati wao wa kutokuwa na shughuli za kilimo, wanashika brashi za kuchora picha. Picha za maua ya Peony zilizochorwa nao zinauzwa vizuri ndani na nje ya China.

Marehemu Guo Tai'an ni "mtu wa kwanza kuchora picha za maua ya peony katika eneo hilo la Pingle". Mwaka 1983, wakati Mji wa Luoyang ulipofanya Maonyesho ya Kwanza ya Maua ya Peony (ambayo ni mtangulizi wa Tamasha la Kitamaduni la Maua ya Peony la Luoyang nchini China), picha ya maua ya peony iliyochorwa na mwalimu huyu wa zamani wa sanaa, ilisifiwa na watu wengi, na wengine waliweka oda maalum.

Ni uzoefu huu ambao ulimfanya kugundua fursa za biashara zilizomo katika uchoraji wa picha za maua ya peony. Wakihamasishwa na Guo Tai'an, idadi kubwa ya wakulima katika kijiji hicho walichukua brashi wakianza kuchora picha. Guo Tai'an alijitolea kufundisha na akaanzisha studio ya kwanza ya uandishi wa kaligrafia na uchoraji picha katika kijiji hicho.

Guo Taisen, mdogo wa kiume wa Guo Tai'an, ni mmoja wa wakulima wa kwanza kujifunza kuchora maua ya peony. Guo Taisen, ambaye ana umri wa miaka 60, anasema, "Kwa kutegemea kazi ya kuchora picha za maua ya Peony, tumefikia lengo dogo la 'kupata yuan milioni 100 kwa mwaka'!"

Mwaka 2011, Bustani ya Ubunifu wa Uchoraji wa Picha za Maua ya Peony ya Pingle China katika kijiji hicho ilikamilika na kuanza kutumika, na wakati huo huo, nembo ya biashara ya "Kijiji cha Kwanza cha Uchoraji wa Picha za Maua ya Peony cha China" ilisajiliwa.

Kwa sasa, kuna wachoraji zaidi ya 1,000 katika bustani hiyo, zaidi ya maduka 150 ya kwenye mtandao wa Taobao yameanzishwa, na timu ya kitaalamu ya utangazaji wa moja kwa moja mtandaoni imepewa mafunzo. Idadi ya wafanyakazi wanaohusika imefikia zaidi ya 2,000. Picha za maua ya peony zilizochorwa na mauzo yake ya kila mwaka zimezidi 500,000, na mapato yake yamefikia Yuan milioni 120.

Bustani hiyo hupokea zaidi ya watalii laki tatu wa makundi au watalii binafsi kutoka ndani na nje ya China kila mwaka. Pingle imeendelea kuwa kijiji kizuri kushughulikia kazi ya urithi wa utamaduni nchini China, ambacho kinahimiza ustawi wa vijijini na kuwahamasisha wakulima wajiendeleze na kupata maendeleo.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha