

Lugha Nyingine
Guizhou, China, "Makumbusho ya Madaraja"
![]() |
Picha hii ikionyesha mandhari ya madaraja matano yanayopita juu ya Mto Wujiang huko Mji wa Zunyi wa Mkoa wa Guizhou, Kusini Magharibi mwa China. (Picha na Tu Min) |
Mkoa wa Guizhou uko kwenye Uwanda wa Juu wa Yunnan-Guizhou, Kusini Magharibi mwa China. Asilimia 93 ya ardhi ya eneo hili ni ya milimani na vilimani, hivyo imeifanya Guizhou kuwa na mandhari nzuri ya kipekee, lakini pia imezuia kupitika kwa njia za wenyeji wa Guizhou kuwasiliana na watu wa nje ya eneo hilo.
Ili kubadilisha kikamilifu hali mbaya ya usafiri wa Guizhou, kuanzia Mwaka 2013, mkoa wa Guizhou umeendeleza kwa nguvu kubwa ujenzi wa barabara. Kufikia Mwaka 2017, kila kijiji huko Guizhou kimepitiwa na barabara. Hivi sasa, Guizhou inachukua nafasi ya nne nchini China kwa kuwa na barabara za mwendo kasi zenye urefu wa kilomita 8,331 na imekuwa kituo cha usafiri kwenye nchi kavu kwa sehemu za Kusini Magharibi mwa China. Mafanikio hayo yanachangiwa na madaraja ya Guizhou.
Kwa mujibu wa takwimu, hivi sasa kuna madaraja zaidi ya elfu 30 yakiwa pamoja na yale yanayoendelea kujengwa kote mkoani Guizhou. Karibu nusu ya madaraja 100 yenye kimo cha juu zaidi duniani yako Guizhou; na manne kati ya madaraja 10 yanayochukua nafasi za mbele kati ya madaraja 100 yenye kimo cha juu zaidi duniani pia yako Guizhou. Na kati ya madaraja tisa nchini China yaliyopewa "Tuzo ya Gustav Lindsay", manne yako mkoani Guizhou. Mafanikio hayo yameifanya Guizhou kuwa "Makumbusho ya Madaraja".
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma