Jenereta ya kwanza ya kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo yafungwa katika eneo la Kizilsu, Mkoa wa Xinjiang China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 24, 2023
Jenereta ya kwanza ya kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo yafungwa katika eneo la Kizilsu, Mkoa wa Xinjiang China
Picha hii iliyopigwa Tarehe 19 Aprili 2023 ikionyesha jenereta ya kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo kabla ya kufungwa katika Eneo linalojiendesha la Kizilsu, Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur, Kaskazini-Magharibi mwa China. Ufungaji wa jenereta ya kwanza ya kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo katika Eneo linalojiendesha la Kizilsu, Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur, China umekamilika Jumamosi asubuhi. (Picha na Liu Zhenlu/Xinhua)

URUMQI - Ufungaji wa mtambo wa kwanza wa kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo katika Eneo linalojiendesha la Kizilsu, Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur, China umekamilika Jumamosi asubuhi.

Kasi ya upepo iliposhuka chini ya mita 6 kwa sekunde Ijumaa usiku, jenereta hiyo yenye uzito wa tani 131 na mapanga matatu ya kuvuna upepo yenye urefu wa mita 95 kila moja, uliinuliwa na makatapila mawili na kuunganishwa kwenye mnara wenye urefu wa mita 110.

Takwimu zilizotolewa na Kampuni ya Nishati ya Longyuan ya China iliyo chini ya Kundi la Uwezekezaji wa Nishati la China zilionesha kuwa, Ukiwa na uwekezaji wa zaidi ya yuan bilioni 1.2 (kama dola za Kimarekani milioni 175), mradi huo unaojumuisha majenereta kama hiyo 38 , utakamilika na kuunganishwa kwenye Gridi ya kitaifa ya China ifikapo robo ya tatu ya mwaka huu, na kuongeza uwezo wa jumla wa uzalishaji wa umeme kwa megawati 200.

Meneja wa mradi huo Qu Qiaogang amesema, mara baada ya mradi huo kukamilika, uwezo wa uzalishaji wa umeme kwa mwaka unakadiriwa kufikia milioni 540 kwh, ambayo inaweza kuokoa tani 164,800 za makaa ya mawe ya kawaida na kupunguza utoaji wa hewa ya kaboni kwa tani 450,000 kila mwaka.

Kwa sasa, umeme wote katika eneo hilo la Kizilsu unazalishwa kwa nishati safi, huku asilimia 60 ya umeme ukiwa unaotokana na nishati ya maji na asilimia 40 unatokana na nishati ya jua. Uwezo wa majenereta ya uzalishaji wa umeme katika Mkoa wa Xinjiang umezidi kilowati milioni 100, ambapo nishati safi inachukua zaidi ya asilimia 40, kwa mujibu wa Gridi ya Taifa ya China, Mkoa wa Xinjiang.

China imeapa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kufuata bila kuyumba njia ya maendeleo ya kijani na utoaji kaboni chache.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha