Mwendesha baiskeli wa kike ahisi kurejea kwenye mazingira ya asili huko Anhui, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 24, 2023

https://english.news.cn/20230423/212fc09c08d84c5894e605be3f81b267/20230423212fc09c08d84c5894e605be3f81b267_202304238133a59494b34be3ae6ee5ae7ffbb81f.jpg

Xie Minyi (wa pili kulia) na wenzake wakishindana kwenye mbio za baiskeli za barabarani za wanawake wazoefu katika Mashindano ya 18 ya Kimataifa ya Wazi ya Uendeshaji Baiskeli ya China Huangshan (Yixian) katika Eneo la Yixian, Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China, Machi 26, 2023. (Xinhua/Zhang Chen)

Eneo la Yixian, mojawapo ya maeneo sita ya Huizhou ya kale, liko kwenye chanzo cha Kusini cha Mlima Huangshan. Mashindano ya 18 ya Kimataifa ya Wazi ya Uendeshaji Baiskeli ya China Huangshan (Yixian) yamekuwa yakifanyika hapa kwa miaka 18 mfululizo, kama chapa ya matukio yanayofungamanisha kwa kiwango cha juu michezo na utalii. Mbio hizo za baiskeli za Huangshan za mwaka huu zilivutia zaidi ya waendesha baiskeli 1,700 kutoka ndani na nje ya China. Xie Minyi, mwendesha baiskeli wa timu ya wanawake ya Neza, alimaliza wa tano katika kipengele cha wazoefu wa mbio za baiskeli za barabarani kwa wanawake. Xie anafanya kazi Shanghai, lakini njia ya baiskeli ya Huangshan ni mojawapo ya njia anazopenda zaidi. Amesema kuwa kuendesha baiskeli huko Huangshan kunamsaidia kupunguza shinikizo la kazi mjini na kumsaidia kupata hisia za kurejea kwenye mazingira ya asili. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha