Biashara kati ya China na Nchi ya Mongolia kupitia Bandari ya Ganqmod yazidi tani Milioni 10 za mizigo ya bidhaa (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 26, 2023
Biashara kati ya China na Nchi ya Mongolia kupitia Bandari ya Ganqmod yazidi tani Milioni 10 za mizigo ya bidhaa
Picha hii iliyopigwa Tarehe 22 Aprili 2023 ikionyesha malori ya mizigo yakiwa chini ya ukaguzi kwenye Bandari ya Ganqmod katika Mji wa Bayannur, Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani wa China. (Xinhua/Li Yunping)

HOHHOT - Kiwango cha biashara kati ya China na Nchi ya Mongolia kupitia Bandari ya Ganqmod, bandari kubwa zaidi ya barabara kuu kati ya nchi hizo mbili, kimezidi tani milioni 10 za mizigo ya bidhaa hadi kufikia sasa mwaka huu, mamlaka ya usimamizi wa bandari hiyo imesema Jumatatu.

Bandari ya Ganqmod ya Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani wa China, ilihudumia mizigo ya bidhaa yenye uzito wa takriban tani milioni 10.02 kuanzia Januari 1 hadi Aprili 22, ikiwa ni wastani wa kila siku wa mizigo ya bidhaa yenye uzito wa tani 112,600.

Bandari hiyo ni bandari ya kwanza ya barabara kuu katika eneo hilo kufikia kiwango cha kuhudumia mizigo ya bidhaa yenye uzito wa tani milioni 10 Mwaka 2023, ikifikia lengo karibu miezi minne mapema kuliko Mwaka 2022.

Ofisi ya mambo ya utawala ya Bandari ya Ganqmod imesema bandari hiyo imekuwa ikifanya juhudi kubwa katika kuinua ufanisi wake wa kupokea na kuidhinisha vibali kwa kutekeleza hatua zaidi za kuwezesha biashara.

Bandari ya Ganqmod ni njia kuu ya kuagiza nishati nchini China, na ni kituo muhimu kwenye ukanda wa kiuchumi wa China-Mongolia-Russia.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha