Samaki pomboo wasio na mapezi waliohamishwa warudi nyumbani kwenye Mto Changjiang (7)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 26, 2023
Samaki pomboo wasio na mapezi waliohamishwa warudi nyumbani kwenye Mto Changjiang
Wafanyakazi wakiwabeba samaki pomboo wasio na mapezi wa Mto Changjiang ambao wataachiliwa kandoni mwa Mto Changjiang katika Mkoa wa Hubei, China, Aprili 25, 2023. (Xinhua/Wu Zhizun)

WUHAN - China siku ya Jumanne kwa mara ya kwanza iliachilia samaki pomboo wanne wasio na mapezi wa Mto Changjiang chini ya uhifadhi wa spishi nje ya mazingira ya asili, ex-situ kwenye Mto Changjiang, ambao ni mto mrefu zaidi wa China, kwa lengo la kuongeza idadi ya spishi hiyo iliyo hatarini kutoweka.

Samaki hao pomboo wasio na mapezi waliotolewa sasa wote walizaliwa katika Hifadhi ya Kitaifa ya Mazingira ya Tian'ezhou iliyo katika Mkoa wa Hubei, katikati mwa China. Ni moja ya maeneo ya uhifadhi wa Samaki hao pomboo wasio na mapezi nje ya mazingira yao ya asili nchini China.

Kati ya hao wanne, pomboo wawili wa kiume wenye umri wa miaka 5 hivi walitolewa katika sehemu ya Xinluo ya Mto Changjiang. Watafiti wametumia miaka miwili kuwasaidia kuzoea na kuendana na mazingira ya asili ya maji ya Mto Changjiang.

Pomboo wengine wawili, mmoja dume mwenye umri wa miaka 13 na jike mwenye umri wa miaka 5, waliachiliwa katika sehemu ya Shishou ya mto huo. Watatengwa kwanza kwa kutumia vyandarua na uwezo wao wa kukamata mawindo utafuatiliwa kabla ya kuongozwa kurudi kwenye eneo la maji ya wazi.

"Hii ni hatua muhimu katika ulinzi wa samaki pomboo wasio na mapezi wa Mto Changjiang, na inaonyesha maendeleo makubwa katika uhifadhi wa spishi nje ya mazingira ya asili," amesema Xia Zhicheng, Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu ya Mkoa wa Hubei.

China ilianza mpango wa kuhamisha pomboo wasio na mapezi katika miaka ya 1990 baada ya wasiwasi kuibuka kuwa idadi ya spishi hiyo ilipungua licha ya hatua za kuwahifadhi.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa kina uliofanyika Mwaka 2022 kuhusu spishi hii, kulikuwa na samaki pomboo wasio na mapezi 1,249 kwenye Mto Changjiang, ikionesha kuongezeka tena kwa spishi hiyo kutoka idadi ya pomboo 1,012 ya Mwaka 2017 pekee.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha