Eneo la makazi ya Xiaoxihu ya Nanjing: "uwanja wa majaribio" ya kuufanya mji mkongwe kuwa mpya katikati mwa mji

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 27, 2023
Eneo la makazi ya Xiaoxihu ya Nanjing:
Maua na majani yakionekana kupitia kuta zilizo na uwazi, kwenye ua ya nyumba ya Qin Liukun huko Nanjing, Mkoa wa Jiangsu, China. (Picha na Ma Taotao/Tovuti ya Gazeti la Umma)

Shangazi Qin Liukun ni mwenyeji wa Mji wa Nanjing, nyumba ya familia yake iliyojengwa zamani iko katika Eneo la makazi ya Xiaoxihu, ambapo ni eneo la kiini cha kusini mwa mji mkongwe wa Nanjing. Ni moja ya maeneo 28 ya kihistoria yaliyowekwa kwenye "Mpango wa Ulinzi wa Mji maarufu wa kihistoria na kiutamaduni wa Nanjing".

Mwaka 2015, Eneo la Makazi ya Xiaoxihu lilianza kufanyiwa ukarabati na ujenzi na limekuwa kama "uwanja wa majaribio" katikati ya mji huo. Mpango huo wa ukarabati unatafuta wazo jipya la kuufanya mji mkongwe kuwa mpya, ukifanya kazi ya "kuhifadhi mtindo wa awali, kujenga upya na kubomoa yasiyotakiwa badala ya "kubomoa makazi kwanza, kujenga upya na kuhifadhi machache".

Huang Jie, naibu meneja mkuu wa Kundi la Uhifadhi na Ujenzi wa Mji wa Kihistoria la Nanjing anasema, "Tunaheshimu matakwa ya wakazi katika kila eneo la nyumba, na tunajitahidi kuwawezesha wakazi wa tangu zamani kusini mwa Mji Mkongwe wa Nanjing waishi maisha kama walivyokuwa katika eneo hilo la makazi baada ya kukarabatiwa upya, wasije wakapoteza uhusiano na ukarabati na ujenzi wa mji".

Mnamo Novemba 26 mwaka jana, Tuzo ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa ya mwaka 2022 ya Uhifadhi wa Urithi wa Utamaduni ya Asia-Pasifiki ilitangazwa rasmi, na Mradi wa ukarabati wa Eneo la Makazi ya Xiaoxihu la Mji wa Nanjing ulishinda Tuzo ya Uvumbuzi wa Usanifu. "Kwa upande wa uvumbuzi wa kijamii na kiteknolojia, mradi huu unatoa uzoefu ambao unaweza kuenezwa na kuigwa." Hii ni tathmini iliyotolewa na waamuzi.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha