Kijiji cha Jiangxiang: “Kielelezo cha Mkoa wa Jiangsu” cha ustawishaji wa vijiji chini ya uongozi wa Chama

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 28, 2023

Nyumba kubwa za wanakijiji wa Jiangxiang. Picha na Yang Wenquan/Mwandishi wa habari wa Tovuti ya Gazeti la Umma.

Nyumba kubwa za wanakijiji wa Jiangxiang. Picha na Yang Wenquan/Mwandishi wa habari wa Tovuti ya Gazeti la Umma.

Katika Kijiji cha Jiangxiang cha Mkoa wa Jiangsu wa China, kuna wanakijiji 900 wa familia 200, miongoni mwao wapo wanachama 101 wa Chama cha CPC , na kamati ya Chama ya kijiji hicho imeanzisha makundi sita ya wanachama. Hivi sasa kijiji hicho kinafanya juhudi ili kuwa “Kielelezo cha Jiangsu” cha ustawishaji wa vijiji chini ya uongozi wa Chama.

Tarehe 24, Aprili, waandishi wa habari walikwenda kwenye kijiji cha Jiangxiang, ambapo katibu wa kamati ya Chama ya kijiji hicho Chang Desheng mwenye umri wa karibu miaka 80 aliwajulisha kuwa, mwaka 2022 wastani ya kipato cha matumizi cha kila mwanakijiji katika kijiji kizima ulifikia Yuan 62,500 (sawa na Dola za Marekani 9028).

“Hivi sasa watu wa familia zote kijijini humo wanaishi kwenye nyumba kubwa, ambazo kila nyumba ni yenye eneo la mita za mraba 220,” amesema Chang, “kijiji chetu kimejenga nyumba hizi kubwa, na ujenzi wa kila nyumba unagharimu zaidi ya Yuan laki 3 (sawa na Dola za Marekani 43,335), na kijiji kinaiuza kwa wanavijiji kwa bei ya Yuan laki 1.28.”

Chang Desheng, katibu wa Kamati ya Chama ya Kijiji cha Jiangxiang, akiwajulisha waandishi wa habari kwenye Jumba la Makumbusho ya Historia ya Kijiji cha Jiangxiang. Picha na Yang Wenquan/Mwandishi wa habari wa tovuti ya Gazeti la Umma.

Katika miaka mingi iliyopita, Kijiji cha Jiangxiang kimeyafanya makundi ya wanachama wa kijiji hicho yatoe mchango ipasavyo katika kuwaongoza wanakijiji kufuata njia ya kustawisha kijiji.

Katika Kijiji cha Jiangxiang, wakulima wanalima mashamba kwa kufuata kilimo cha jadi bila kutoa uchafuzi kwa mazingira, kwa mfano kupanda mimea yenye kiasi kikubwa cha Nitrogen, Phosphorus na Potassium ili kuongeza rutuba ya mashamba ya mpunga; kupanda mpunga mara moja tu kila mwaka ili kupumzisha mashamba, na kufuga batabukini wakati wa mapumziko ya msimu wa kilimo…… mwaka 2022 faida za kilimo za kila 1/15 hekta kwenye mashamba ya Kijiji cha Jiangxiang zilifikia Yuan 2,500 hivi (sawa na Dola za Marekani 360.92).

Mwanakijiji wa Jiangxiang akionesha udongo  mweusi wenye rutuba nyingi kwenye mashamba ya mpunga. Picha na Yang Wenquan/Mwandishi wa habari wa tovuti ya Gazeti la Umma.

Mwanakijiji wa Jiangxiang akionesha udongo mweusi wenye rutuba nyingi kwenye mashamba ya mpunga. Picha na Yang Wenquan/Mwandishi wa habari wa tovuti ya Gazeti la Umma.

Licha ya hayo, katika miaka ya karibuni iliyopita, kijiji hicho kimewekeza karibu Yuan Milioni 40 kujenga kituo cha matibabu na utunzaji wa wazee cha Jiangxiang kinatumia mfumo wa “ujenzi wa kiumma na uendeshaji wa kibinafsi”, na kimetoa huduma mbalimbali kwa wakazi wazee wa kijiji hicho.

Picha hii ikionesha Mfano wa mpango wa maendeleo ya Kijiji cha Jiangxiang. Picha na Yang Wenquan/Mwandishi wa habari wa Tovuti ya Gazeti la Umma

Picha hii ikionesha Mfano wa mpango wa maendeleo ya Kijiji cha Jiangxiang. Picha na Yang Wenquan/Mwandishi wa habari wa Tovuti ya Gazeti la Umma

Habari husika:

Eneo la makazi ya Xiaoxihu ya Nanjing: "uwanja wa majaribio" ya kuufanya mji mkongwe kuwa mpya katikati mwa mji

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha