Vijana wa China wajitolea katika miradi ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) nchini Bangladesh

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 05, 2023
Vijana wa China wajitolea katika miradi ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) nchini Bangladesh
Yao Yao (wa kwanza kulia), meneja wa fedha wa Kampuni ya Ushirikiano wa Uchumi na Teknolojia ya China Shandong, tawi la Asia-Pasifiki akifanya kazi katika mradi wa Barabara ya Mwendokasi ya Dhaka huko Dhaka, Bangladesh Mei 3, 2023.(Xinhua)

DHAKA - Katika kijiji cha Dasherkandi, kilicho karibu na Mji Mkuu wa Bangladesh, Dhaka, watoto wa eneo hilo walikuwa wakiogelea kwa furaha katika mto safi chini ya jua kali. Deng Mingze, naibu meneja wa Mtambo wa Kusafisha Maji taka wa Dasherkandi, alihisi furaha alipotazama tukio hili.

"Mambo yalikuwa tofauti kabisa hapo awali," ameeleza mhandisi huyo wa China mwenye umri wa miaka 33 kutoka kampuni ya uhandisi ya PowerChina ya Chengdu, China huku akiongeza kuwa maji taka ambayo hayajasafishwa yalikuwa yakiingia moja kwa moja kwenye mto huo, na kuufanya kuwa mchafu siku za nyuma.

Mtambo wa Kusafisha Maji taka wa Dasherkandi, uliofadhiliwa na Benki ya Uuzaji na Uagizaji Nje ya China (Exim China) na kujengwa na Kampuni ya HydroChina, ambayo ni kampuni tanzu ya PowerChina, ulianza kufanya kazi Aprili 2022. Huo ni mtambo wa kwanza wa kisasa wa kusafisha maji taka nchini Bangladesh, wenye uwezo wa kutoa huduma za kisasa za kusafisha maji taka kwa takriban watu milioni 5 huko Dhaka.

Kuanzia wakati huo, maji yote yanayotiririka mtoni yamesafishwa, hivyo yanafanya mto kuwa wazi na kuonekana kwa macho, amesema Deng, huku akieleza kuwa watoto hucheza katika eneo hilo.

Huko Keraniganj, katika kitongoji cha Dhaka, Zhang Yadong, mhandisi kutoka Shirika la Reli la China, anafanya kazi pamoja na wafanyakazi wenzake wenyeji kwenye mradi mkubwa zaidi wa reli ya BRI nchini Bangladesh.

Mapema Aprili mwaka huu, mradi huo unaofadhiliwa na Benki ya Uuzaji na Uagizaji Nje ya China na kujengwa na Shirika la Reli la China, ulifanya majaribio yenye mafanikio ya kupitisha treni.

Katika miaka ya hivi karibuni, Bangladesh imeshiriki kikamilifu katika BRI na imeshirikiana na China katika miradi mingi ya miundombinu, ikiwa ni pamoja na Barabara ya Mwendokasi ya Dhaka.

Mradi huo unatarajiwa kuajiri zaidi ya watu 10,000 wakati wa ujenzi na kupunguza muda wa kusafiri kutoka uwanja wa ndege hadi barabara kuu ya kitaifa ya N1 ya Bangladesh hadi takriban robo ya muda wa awali wakati utakapozinduliwa na kuanza kufanya kazi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha