Daktari wa mifugo vijijini wa China anayevalia na kutumia vifaa vya rangi ya waridi apata umashuhuri na kuokoa mifugo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 08, 2023
Daktari wa mifugo vijijini wa China anayevalia na kutumia vifaa vya rangi ya waridi apata umashuhuri na kuokoa mifugo
Daktari wa Mifugo Bai Hua akishona jeraha la ng'ombe anayemilikiwa na mwanakijiji katika Eneo la Yuanzhou huko Guyuan, Mkoa unaojiendesha wa Ningxia nchini China, Aprili 18, 2023. (Xinhua/Feng Kaihua)

YINCHUAN – Msichana mwenye umri wa miaka 27, daktari wa mifugo vijijini mwenye ujuzi anayeishi katika Mji wa Guyuan, Mkoa unaojiendesha wa Ningxia, Kaskazini-Magharibi mwa China, anashikilia nafasi mbili kama daktari wa mifugo na mtu mashuhuri wa mtandaoni ambaye amepata jumla ya wafuasi milioni tatu kwenye majukwaa mengi ya mtandaoni ya kushiriki na kutangaza moja kwa moja kwa njia ya video, kama vile Kuaishou, Bilibili na Douyin ya China.

Katika video zake fupi, tunaweza kuona kuwa Bai Hua yuko katika mazizi machafu ya ng'ombe, lakini anabaki kuwa mrembo na mwenye mtindo huku akiendelea kutibu ng'ombe waliougua kwa utulivu, akizalisha vichanga vya ng'ombe, na kuchoma sindano. Tofauti kubwa ya mtindo wa kimaisha inayovutia mapenzi ya mashabiki wake.

Daktari huyo wa mifugo kijana wa kike, ambaye ni adimu kujihusisha katika taaluma chafu, yenye harufu mbaya na hatari kwa kiasi fulani, alijua haikuwa chaguo rahisi kwake kufanya kazi ya namna hiyo.

Licha ya kurushiwa samadi ya ng'ombe usoni huku akivuta mkia wa ng'ombe, na kupigwa teke na ng'ombe mara nyingi, mwanamke huyo anayejali sana taswira hajawahi kuwa na mawazo ya kubadilisha kazi. Badala yake, bado amedhamiria kupiga mbizi kwa kina katika sayansi ya mifugo, na kuwa na ndoto za kuwa daktari wa mifugo anayeongoza.

Bai hakuonesha dalili zozote za kuvunjika moyo na tamaa yake ya umashuhuri, hali ambayo ilimtia moyo kutotafuta kazi ya pili. "Nataka kuwasaidia vijana wengi zaidi kupata mtazamo wa karibu wa taaluma hii kupitia mfano wangu. Nataka wafahamu kuwa madaktari wa mifugo pia wanaweza kuvaa mavazi safi na maridadi kila siku, na kazi hiyo inaweza kuvutia. Hii itahimiza vijana wengi zaidi kujiunga nami."

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha