Kenya yaandaa mashindano ya Kungfu huku kukiwa na kuongezeka kwa umaarufu wa mchezo huo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 08, 2023
Kenya yaandaa mashindano ya Kungfu huku kukiwa na kuongezeka kwa umaarufu wa mchezo huo
Wachezaji wa Kungfu wakifanya mazoezi katika Kaunti ya Kiambu karibu na Nairobi, Kenya, Mei 6, 2023. (Xinhua/Wang Guansen)

NAIROBI - Kenya Jumamosi iliandaa mashindano ya Kungfu katika mji wa kati wa Kenya wa Kiambu uliopo vitongoji vya Nairobi, mji mkuu wa Kenya.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Kungfu la Kenya Ngaruiya Njonge amesema kuwa vilabu 13 na washindani 70 walishiriki katika awamu ya pili ya Mashindano ya Ubingwa wa Kungfu ya Kenya ambayo yamefadhiliwa na ubalozi wa China nchini Kenya.

"Mashindano haya ni sherehe ya utamaduni tajiri na mahiri wa Kungfu Wushu, mchezo ambao umevutia watu kote duniani," amesema Njonge.

Ameongeza kuwa Kungfu ilianza kuendelezwa nchini Kenya Mwaka 2000 na kwa sasa, inakadiriwa Wakenya 3,000 wanashiriki kikamilifu katika mchezo huo.

Awamu ya kwanza ya Mashindano ya Ubingwa wa Kungfu ya Kenya Mwaka 2021 lilisaidia kutengeneza shauku zaidi katika mchezo huo nchini Kenyea, kwa mujibu wa Njonge.

Tang Jianjun, Konsela wa Utamaduni wa ubalozi wa China nchini Kenya, amesema kuwa mchezo wa Kungfu Wushu, aina ya uwasilishaji mawazo ya jadi ya Wachina, sasa umeibuka kuwa mchezo wa kimataifa unaojumuisha nchi na kanda 158 katika mabara matano.

"Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki imeidhinisha Kungfu Wushu kujumuishwa kama mchezo rasmi katika Michezo ya nne ya Olimpiki ya Vijana huko Dakar Mwaka 2026. Ninatumai wakati huo, wachezaji wa Wushu wa Kenya watasimama kwenye hatua ya Olimpiki ya vijana na kupata matokeo mazuri," amesema Tang.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha