Habari Picha: Eneo la mandhari nzuri la Kasri la Huaqing huko Xi'an, Kaskazini mwa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 11, 2023
Habari Picha: Eneo la mandhari nzuri la Kasri la Huaqing huko Xi'an, Kaskazini mwa China
Picha hii ikionyesha watalii wanaotembelea eneo lenye mandhari nzuri la Kasri la Huaqing huko Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, Kaskazini-Magharibi mwa China, Mei 5, 2023. (Xinhua/Liu Xiao)

Xi'an, mji wenye historia ya miaka zaidi ya 3,100, ulikuwa mji mkuu katika enzi za kifalme 13 katika historia ya China. Pia ni eneo maarufu la kufukuliwa kwa sanamu za askari na farasi zilizofinyangwa katika Enzi ya Qin (221-207 KK).

Kama moja ya alama za kitamaduni huko Xi'an, Kasri la Huaqing, ambalo ni eneo la mapumziko la zamani la wafalme wa Enzi ya Tang (618-907), liko chini ya Mlima Lishan. Kasri hilo ni maarufu kwa hadithi maarufu ya mapenzi ya Mfalme wa Tang, Li Longji na waridi wake kipenzi Yang Yuhuan. Pia ni eneo linalojulikana la Tukio la Xi'an ambalo ni tukio maarufu la kihistoria.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha