Mradi mkubwa wa kupeleka maji kutoka kusini hadi kaskazini unanufaisha zaidi ya watu milioni 150

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 15, 2023
Mradi mkubwa wa kupeleka maji kutoka kusini hadi kaskazini unanufaisha zaidi ya watu milioni 150
Picha hii iliyopigwa Tarehe 12 Mei 2023 ikionyesha kituo cha kusukuma maji cha Mradi wa Kupeleka Maji kutoka Kusini hadi Kaskazini katika Eneo la Sihong, Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China. Njia za mashariki na kati za Mradi wa Kupeleka Maji kutoka Kusini hadi Kaskazini mwa China zimenufaisha zaidi ya watu milioni 150, kampuni ya China ya Mradi wa Kupeleka Maji kutoka Kusini hadi Kaskazini imesema Jumapili. Mradi huo umepeleka mita za ujazo bilioni 62 za maji hadi maeneo ya kaskazini mwa China yenye ukame kupitia njia za mashariki na kati, kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo. (Picha na Fang Dongxu/Xinhua)

BEIJING - Njia za mashariki na kati za Mradi wa Kupeleka Maji kutoka Kusini hadi Kaskazini mwa China zimenufaisha zaidi ya watu milioni 150, kampuni ya China ya Mradi wa Kupeleka Maji kutoka Kusini hadi Kaskazini imesema Jumapili.

Mradi huo umehamisha maji yenye mita za ujazo bilioni 62 hadi maeneo ya kaskazini mwa China yenye ukame kupitia njia za mashariki na kati, kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo.

Mradi wa Kupeleka Maji kutoka Kusini hadi Kaskazini nchini China una njia tatu. Njia ya kati ndiyo maarufu zaidi, inayoanzia kwenye Hifadhi ya Danjiangkou katika Mkoa wa Hubei, Katikati mwa China na kuvuka Henan na Hebei kabla ya kufika Beijing na Tianjin. Ilianza kusambaza maji Mwezi Desemba 2014.

Njia ya mashariki inapeleka maji kutoka Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China hadi maeneo mbalimbali yakiwemo Tianjin na Shandong.

Njia ya magharibi iko katika hatua ya mipango na bado haijajengwa.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha