Timu ya Mpira wa Kikapu ya Mkoa wa Liaoning yashinda taji lake la tatu la Ligi ya Kikapu ya China CBA katika historia (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 16, 2023
Timu ya Mpira wa Kikapu ya Mkoa wa Liaoning yashinda taji lake la tatu la Ligi ya Kikapu ya China CBA katika historia
Kyle Fogg wa Timu ya Mpira wa Kikavu ya Liaoning Flying Leopards akishangilia wakati wa mechi ya mwisho ya raundi ya nne kati ya Liaoning Flying Leopards na Zhejiang Golden Bulls katika mchezo wa mchujo wa Fainali ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Kikapu la China (CBA) msimu wa 2022-2023, huko Shenyang, Mkoa wa Liaoning, Kaskazini mwa China, Mei 15, 2023. (Xinhua/Wu Zhuang)

SHENYANG, China - Mabingwa watetezi Timu ya Liaoning Flying Leopards kutoka Mkoa wa Liaoning wa China imeipiga Timu ya Zhejiang Golden Bulls kutoka Mkoa wa Zhejiang pointi 106-70 katika Mchezo wa 4 wa Fainali za Shirikisho la Mpira wa Kikapu la China (CBA) Jumatatu, na kushinda mfululizo wa mechi 4-0 na kunyakua kombe lake la tatu la Ligi ya CBA.

Mlinzi wa pointi wa Liaoning Zhao Jiwei ametunukiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Fainali (FMVP).

Ikiwa imezungukwa na shangwe za mashabiki wapatao 10,000 waliokuwa wamevalia fulana za kijani ambayo ni rangi ya timu hiyo ya Liaoning, Timu ya Flying Leopards ilionyesha ari kubwa ya kushinda, ikiuanza mchezo huo kwa kuwa na shinikizo kubwa ya kujilinda na kuweka msimamo hadi mwisho wa mchezo. Mchezaji Kyle Fogg tena amekua mchezaji muhimu kwani alifunga pointi 17 na kupoka mpira wachezaji wa timu mpinzani mara tano pekee ndani ya dakika 17.

Flying Leopards wamewahi kutawazwa mabingwa wa Ligi ya CBA katika misimu ya CBA ya 2017-18 na 2021-22.

Kocha mkuu wa Timu ya Liaoning, Yang Ming amesema kuwa ubingwa wa msimu huu umekuwa mgumu zaidi kupata, "Nataka kushukuru juhudi za kila mtu kwa timu. Umekuwa msimu mgumu. Liaoning inavutia umakini wa hali ya juu, na nilikuwa chini ya shinikizo kubwa. Lakini tumebadilisha shinikizo kuwa nguvu yetu , hasa wachezaji wakongwe, wana hisia bora za dhamira."

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha