Maonyesho ya China na nchi za Ulaya Mashariki na Kati (CEEC) yaanza, yavutia waonyeshaji 380 kutoka CEEC

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 17, 2023
Maonyesho ya China na nchi za Ulaya Mashariki na Kati (CEEC) yaanza, yavutia waonyeshaji 380 kutoka CEEC
Picha hii iliyopigwa Tarehe 16 Mei 2023 ikionyesha bidhaa zikionyeshwa kwenye Maonyesho ya China na Nchi za Ulaya Mashariki na Kati (CEEC) huko Ningbo, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China. (Xinhua/Huang Zongzhi)

NINGBO - Maonyesho ya Tatu ya China na Nchi za Ulaya Mashariki na Kati (CEEC) na Maonyesho ya Kimataifa ya Bidhaa za Watumiaji yameanza mjini Ningbo, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China siku ya Jumanne. Maonyesho hayo ya mwaka huu ya China na CEEC yamevutia waonyeshaji zaidi ya 380 wa nchi za Ulaya Mashariki na Kati. Zaidi ya wanunuzi 2,000 wamejiandikisha kwa ajili ya maonyesho hayo, huku idadi ya washiriki ikitarajiwa kuzidi 100,000.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha