Uchumi wa usiku washamiri huko Yuncheng, Mkoa wa Shanxi wa China mapema katika majira ya joto (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 17, 2023
Uchumi wa usiku washamiri huko Yuncheng, Mkoa wa Shanxi wa China mapema katika majira ya joto
Watu wakifurahia wikendi kwenye eneo la kupiga kambi katika kitongoji cha Dongguo, Wilaya ya Yanhu katika Mji wa Yuncheng, Mkoa wa Shanxi, Kaskazini mwa China, Mei 13, 2023. (Picha/Yan Xin)

Uchumi wa usiku umeshamiri katika Wilaya ya Yanhu iliyoko Mji wa Yuncheng, Mkoa wa Shanxi, Kaskazini mwa China mapema katika majira ya joto. Kwa wananchi wenyeji ambao wanataka kuwa karibu na mazingira asilia na kufurahia wakati wao wa likizo kwenye mazingira asilia, kupiga kambi kumekuwa chaguo maarufu.

Katika miaka ya hivi karibuni, Mji wa Yuncheng umeboresha miundombinu yake ya ndani na kuhimiza shughuli za matumizi kwenye manunuzi ya usiku kama vile kula chakula migahawani, kusafiri na shughuli za kitamaduni na burudani, ili kujaribu kutumia kikamilifu uwezo wa matumizi katika manunuzi ya usiku, kuhimiza maendeleo ya kiuchumi na kuongeza uhai wa mji.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha