Rais Xi afanya karamu ya kukaribisha viongozi wa Nchi za Asia ya Kati katika mji wa kihistoria wa Njia ya Hariri kwa mkutano wa viongozi wakuu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 19, 2023
Rais Xi afanya karamu ya kukaribisha viongozi wa Nchi za Asia ya Kati katika mji wa kihistoria wa Njia ya Hariri kwa mkutano wa viongozi wakuu
Rais Xi Jinping wa China na mkewe Peng Liyuan wakiwa kwenye picha ya pamoja na wageni mbele ya Mnara wa Ziyun huko Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, Kaskazini-Magharibi mwa China, Mei 18, 2023. (Xinhua/Ding Haitao)

XI'AN - Rais Xi Jinping wa China na mkewe Peng Liyuan wameandaa karamu ya kuwakaribisha wageni waliokusanyika huko Xi'an, mahali pa kuanzia kihistoria kwa Njia ya kale ya Hariri, kuhudhuria mkutano wa kihistoria wa viongozi wakuu wa China na Nchi za Asia ya Kati.

Mkutano huo ulioanza jana Alhamisi na unaendelea leo Ijumaa, ni mkutano wa kwanza wa ana kwa ana kati ya viongozi wakuu wa China na nchi tano za Asia ya Kati tangu China ianzishe uhusiano wa kidiplomasia na nchi hizo miaka 31 iliyopita.

Kuanzia Jumatano hadi Alhamisi, Rais Xi alikutana au kufanya mazungumzo na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev, Rais wa Tajikistan Emomali Rahmon, Rais wa Kyrgyzstan Sadyr Japarov, Rais wa Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev na Rais wa Turkmenistan Serdar Berdimuhamedov.

Rais Xi amewaandalia karamu viongozi hao siku ya Alhamisi jioni katika Mnara wa Ziyun, au mnara wa wingu zambarau kwa Kiingereza. Ukiwa umeng’arishwa kwa taa nyekundu za kijadi, mnara huo uko katika Paradiso ya Tang, muundombinu ambao umejengwa kwenye eneo la mabaki ya asili ya kale ya kifalme yaliyoanzia Enzi ya Tang (618-907).

Rais Xi amesema, licha ya mabadiliko ya hali ya kimataifa, China na nchi za Asia ya Kati zimekuwa zikiheshimiana, zimefurahia ujirani mwema, zimefanya kazi kwa ushirikiano kwa manufaa ya pande zote mbili, na kuendelea kupiga hatua za kihistoria katika kuinua uhusiano.

Karamu ya Kitamaduni

Xi'an, mji ulioanzishwa miaka zaidi ya 3,100 iliyopita, ulikuwa mji mkuu wa enzi 13 za kifalme katika historia ya China, ikiwa ni pamoja na Enzi ya Tang, wakati mji huo ulipokuwa ukijulikana kwa jina la Chang'an.

Wakati wa utawala wa Enzi ya Tang, mji huo ulivutia idadi kubwa ya wafanyabiashara, wajumbe, na wanafunzi wa kigeni. Wengi wao walikuwa kutoka nchi za sasa za Asia ya Kati.

Mji huo pia ni mahali ambapo mjumbe wa China Zhang Qian alitumwa mara mbili kwenda Asia ya Kati kwa ujumbe wa amani na urafiki miaka zaidi ya 2,100 iliyopita, akianzisha Njia ya Hariri inayounganisha Mashariki na Magharibi, Asia na Ulaya.

“Katika milenia iliyopita, watu wa China na wa Asia ya Kati wameunda utukufu wa Njia ya kale ya Hariri na kuandika sura nzuri katika historia ya mabadilishano kati ya ustaarabu,” Rais Xi amesema.

Rais Xi alipendekeza wazo la kujenga "ukanda wa kiuchumi kando ya Njia hiyo ya kale ya Hariri" katika nchi ya Kazakhstan Mwaka 2013, pendekezo ambalo, liliunganishwa pamoja na pendekezo la Njia ya Hariri ya baharini ya Karne ya 21, na hatimaye ikawa Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha