Miradi yenye thamani ya zaidi ya yuani bilioni 290 yatiwa saini katika Maonyesho ya Magharibi ya China (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 19, 2023
Miradi yenye thamani ya zaidi ya yuani bilioni 290 yatiwa saini katika Maonyesho ya Magharibi ya China
Watu wakitembela Maonyesho ya Tano ya Kimataifa ya Uwekezaji na Biashara ya China Magharibi katika Mji wa Chongqing, Kusini-Magharibi mwa China, Mei 18, 2023. (Xinhua/Huang Wei)

CHONGQING – Makubaliano ya uwekezaji kwenye miradi mikubwa 88 yenye thamani ya yuan bilioni 290.7 (kama dola za kimarekani bilioni 41.55), yametiwa saini kwenye Maonyesho ya Tano ya Kimataifa ya Uwekezaji na Biashara ya China Magharibi, ambayo yameanza Alhamisi katika mji wa Chongqing, Kusini Magharibi mwa China.

Kati ya miradi hiyo, 84 itapatikana Chongqing, ikiwa na makubaliano ya uwekezaji ni yenye thamani ya yuani bilioni 285.42, na kati yake, 56 imezidi thamani ya yuani bilioni 1 kila mmoja, ikichukua asilimia 66.7 ya miradi yote ya kandarasi iliyotiwa saini huko Chongqing.

Miradi hiyo inashughulikia nyanja mbali mbali kama vile magari yanayotumia nishati mpya yaliyounganishwa teknolojia za akili bandia, vifaa vya teknolojia ya hali ya juu, vifaa vinavyotumia teknolojia za akili bandia, nishati, na usindikaji wa chakula na bidhaa za kilimo.

Maonyesho hayo yanayofanyika kwa siku nne yakiwa na kaulimbiu isemayo "Kuungana Mikono na Magharibi kwa mustakabali Mzuri zaidi," yamevutia zaidi ya kampuni 900 kutoka nchi na kanda 38, na maeneo 26 ya ngazi ya mkoa kote nchini China.

Malaysia ni nchi mgeni wa heshima mwaka huu na mikoa ya magharibi ya Sichuan na Gansu ya China ni wageni wa heshima wa ngazi ya mkoa. Maonyesho na makongamano yanayohusu mada mbalimbali na shughuli za utangazaji bidhaa zitafanyika wakati wa tukio hilo.

Takwimu zilizotolewa na kamati ya biashara ya Chongqing zinaonyesha kuwa jumla ya miradi 945 ilitiwa saini wakati wa maonyesho manne ya awali, ikiwa na uwekezaji wenye thamani ya jumla ya yuani trilioni 1.66.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha